INAUZWA Nauza Viwanja, nyumba na Mashamba Kigamboni Dar es Salaam

Hizi rangi zimenifanya nirudie tena kusoma location, nkadhan iko mbagala chamanzi
 
Wewe utaishi wapi? Nashauri ikamilishe uishi chini chumba cha huu pangisha hata kwa laki maisha yataenda
 
Ni nzuri ila kwa hiyo hela at least ingekuwa imekamilika, hapo utapata hela ndogo. Tafuta hela upige rangi na hapo nje weka pavings na kigarden cha kimtindo, utauza fasta tena bei nzuri.
Mtu hawezi kutoa zaidi ya mil 150 halafu bado aje kupambana na mafundi, anatakiwa ahamie tu.
 
Sio yake mkuu,ni dalali.
 
Mkuu nakushauri usiuze hiyo nyumba komaa tu uimalize au uhamie hivyo hivyo. Najua uenda una matatizo unahitaji pesa ila komaa na dunia hiyo nyumba usiiuze. Kama ni ada hamisha watoto shule peleka za kawaida na jishushe kimaisha ila mjengo baki nao ndio urithi mkubwa wa watoto. Siku hizi tunawasomesha na kazi hawapati so elimu sio urithi mkubwa kihivyo kama mali kama hii nyumba.

Ramani yako nzuri sana pambana uimalize
 
Nakubaliana nawe kwamba siku hizi kusomesha na kusema eti umemuachia urithi mtoto ni kujidanganya. Lazima umuachie mijengo plus elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…