Dr. Bashiru uzuri wake ni kwamba ni mchapa kazi sana, ana kipaji cha juu sana cha organisation, pia hana umri mkubwa!
CV yake imepanda sana na anayo elimu. Ukiangalia hayo pekee, na jinsi alivyo bakishwa kwenye system, tegemea kuwa Dr Bashiru bado anahitajika sana na ni akiba - watawala wanayo tegemea.
Mfano: Dr. Bashiru hapendwi haswa na wapinzani kwa sababu alisaidia CCM kushinda viti vyote vya ubunge na uraisi - wanavyo dai! Je! Chaguzi zimeisha? Je CCM haitaki kushinda tena? Je! Dr. Bashiru hatahusishwa kamwe kufanikisha hili tena? Mpunguze mihemko yenu kusudi msije kukumbana na maneno haya - "msiye mpenda kaja"!