Navyoona si Bashiru si Polepole hawana nguvu tena, wanagugumia tu

Tumia neno kuiba uchaguzi, acha kuzunguka kama taga
 
Mwenye CV ya H. Pole pole tafadhali
 
Tuliomba Sana na kufunga Ili Mungu awaaaibishe wale wote watakaovuruga uchaguzi mkuu 2020 hakika ametenda tumeuona ukuu wake,wataendelea kuabishwa bado mahela na tume yake, waliwanyima watz haki zao ya msingi za kuwachagua wawakilishi wao.
Mwanakondoo ameshinda.......
Uchaguzi Mkuu Ingekuwa ni gharama nafuu tungeomba urudiwe Ili tupate wawakilishi wetu.
 
Hawa ndo walikuwa madalali wa kununua waunga juhudi na pia ndio vinara wa siasa chafu za kupita bila kupingwa.Wamejitengenezea pesa nyingi Sana kwenye udalali wa kununua wapinzani na pia malipo ya wasanii Ili kuwajaza watz wapate burudani za bure
 
Hawa jamaa kwisha habari yao...ni wa kuhurumia...hawa ni wa kuwatuma kina kibajaji na msukuma eti wakajenge hoja ya Legacy ya Mwendazake kweli?
 
Mnazikumbukaga hiz nyimbo yakishawakumba.
Mkiwa juu ya mstari walaaaa mna banjuka tu na kubanjua wanyonge ..... tulien hivyo hivyo

Hehehe Mkuu haya mambo acha tu,,

Madaraka matamu sana, ukiyapata huwezi kuamini kuwa ipo siku utarudi chini.
 
Hivi wewe mtu mzima na akili zako timamu,umebaki kuwa na wivu wa kipumbavu inakusaidia nini?,una kipi cha kuwazidi hao jamaa? Umekalia majungu na umbea ambao haukusaidii katika maisha yako,hebu fanya kazi yako kujiingizia kipato na kujikwamua kimaisha!
 
Mwendazake ndo alikua akiwapa kiburi Sasa hizi Ni Zama mpya.acha wapambane na Hali zao
 
Wewe naweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! Hujui humu twatoa stress! Kama Bashi ni uncle wako basi washwa vema!
 
Sasa huo ushindi alippatia CCM ni kwamba alitumia akili sana ? Yaani kitendo cha kuwaita wakurugenzi wa halmshauri na wakuu wa wilaya na kuwaaguza akikisheni kila mgombea wa CCM anashinda katika kila kituo cha kupigia kura nayo ni akili kubwa? Si hata mtoto wa darasa la saba anaiweza hii? Kama ana uwezo mkubwa aamie upinzani ambapo hakuna sapoti ya dola uone ataambulia nini?
 
Tokea kutambulishwa ulipaji wa kutumia controller number kwenye mali za CHAMA, basi umetokea kumchukia Dr Bashiru
 
Huu uzi umeuandika ukiwa uwanja wa fisi na kombe lako la gongo mkononi, au ulikuwa msalani unakata gogo huku unaandika yanayokujia kichwani kwako? Maana hakuna anaeelewa ulichoandika hapa
Hahahaha masimamngo tu.. ila acha waliwasimanga wenzao. Hamna namna.
 
Ameharibu sana utamaduni wa nchi yetu - yaani utawala wa awamu ya tano hamna ubishi ni UTAWALA ULIOJIPACHIKA MADARAKANI. Ndiyo maana ikabidi hata Mwendazake atolewe kafara! Hovyo kabisa!
Atolewe kafara!!?
 
Eti CV yake imepanda!!!!. CV ya kutumia nguvu ya dola na kununua watu waunge juhudi kwa kutumia kodi ya waTanzania. Kwa uelewa wako umeishia hapo kuelewa kwamba, vyama vya Upinzani vimekosa wabunge bungeni kwa masanduku ya kura, hadi Ndugai na Mahera wakaamua kuwapeleka Covid 19 bungeni? Nadhani kwa level yako ya kuelewa, huwezi kuelewa kwa nini KATIBA imebidi ikanyagwe ili hawa Covid 19 wawepo bungeni.
 
Yaani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…