Nawaelewa Wapentekoste/Walokole wanapofurahia kuketi moja meza na wakuu. Free Pentecost

Nawaelewa Wapentekoste/Walokole wanapofurahia kuketi moja meza na wakuu. Free Pentecost

Wapentekoste waliingia Tanganyika zamani sana miaka ya kati ya 1900's. Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) walianza kuwepo Tanzania mwaka 1932, hata hivyo hawakuweza kupata mafanikio makubwa mpaka miaka ya mwishoni ya 1980 na mwanzoni miaka ya 1990. Walipoanza kuingia kwa nguvu katika jamii walionekana watu wavurugaji tu na wapiga kelele hadi wakabatizwa jina la kejeli la "walokole".

Hata hivyo kadri muda ulivyoendelea waliendelea kuvuna wafuasi kutoka Katoliki, Lutheran, Anglican hadi na Uislamu, taratibu nao wakaanza kuchukuliwa kwa uzito na heshima kubwa katika jamii, mwishowe wakaweza kupenya hadi kwa watawala wa nchi na kuwa sehemu muhimu ya ushiriki wa siasa za nchi, wakapewa kipaumbele katika viti vya mbele vya nchi na hadi sasa kufikia kuwa karata turufu ya kisiasa katika nchi. Kwa safari hii ndefu na mahangaiko mikubwa sana waliyopitia ni vigumu wao kujiondoa katika karamu kutoka meza kuu kwa sasa, tuwavumilie na kuwaelewa tu, ni wakati wao wa kula nao.
Kuna kitu kikubwa sana umechanganya, hapa nitakuelewesha.

Ulokole wa zamani, kwa sehemu kubwa umekufa na kufifia. Mengi ya haya makanisa ya kilokole yanayochipuka sasa yako kibagani, hayana kabisa ile sense ya upentekoste, yamekaa kitapeli na kiuganga uganga. Haya yako tayari kukaa na yoyote ili kulinda utapeli wao. Yanatumia mwamvuli wa upontekoste ili kuficha yanayoendelea nyuma ya pazia.

Lengo halisi la upentekoste halisi tangu ulipoingia Tanzania hapo zamani ilikuwa ni kutengeneza waumini halisi wa kikristo kutoka kwenye mifumo ya kibagani na kidini. Lengo lile taratibu lilianza kubadilika na kuwa, kuvuna waumini kutoka angle yoyote ili kujijenga binafsi kwa maslahi ya sadaka.
 
Ulokole ndio huo huo, sema kulitokea mabadiliko makubwa mbalimbali na ya kasi katika sehemu kubwa ya mfumo wake ikiwemo mavazi, muziki na namna ya waumini wake kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii, siasa na uchumi. Lakini pia mabadiliko makubwa yamewezekana ndani ya ulokole kwa sababu hauko centralised kama makanisa traditional ya RC, KKKT na Anglican
 
Nimependa ulipoeleza neno walokole. Watu wengi hawaelewi asili ya neno hili, hudhani ulokole ni dini, dhehebu na imani, kumbe ilikuwa ni neno la kejeli, dhihaka na dharau kwa wapentekoste. Huwa nashangaa sana mpentekoste kuitwa na kujiita mlokole, kumbe ni neno la kejeli tu

Hii combination ya sasa sio ya wapentekoste wote. Kumbuka wale wanaopigwa pale Ubungo nao ni wapentekoste. Hawa wana makundi yanaibuka kila uchao. Na kwa sababu hiyo, hata organisation yake imekuwa ngumu mno. Kila anayepata upenyo, anautumia ipasavyo.

Tofauti na nguli wao. Wako very organised. Na hata sasa wapo ndani kabisa wanaangalia na wanajua kila kinachoendelea.

Kukaa kwao pembeni ni moja ya strategy kubwa za kivita, na zinawaumiza sana baadhi ya watu. Maana wanajua fika, usimchezee simba aliyelala ukadhani ni dume la nyani.
 
Kuna kitu kikubwa sana umechanganya, hapa nitakuelewesha.

Ulokole wa zamani, kwa sehemu kubwa umekufa na kufifia. Mengi ya haya makanisa ya kilokole yanayochipuka sasa yako kibagani, hayana kabisa ile sense ya upentekoste, yamekaa kitapeli na kiuganga uganga. Haya yako tayari kukaa na yoyote ili kulinda utapeli wao. Yanatumia mwamvuli wa upontekoste ili kuficha yanayoendelea nyuma ya pazia.

Lengo halisi la upentekoste halisi tangu ulipoingia Tanzania hapo zamani ilikuwa ni kutengeneza waumini halisi wa kikristo kutoka kwenye mifumo ya kibagani na kidini. Lengo lile taratibu lilianza kubadilika na kuwa, kuvuna waumini kutoka angle yoyote ili kujijenga binafsi kwa maslahi ya sadaka.

Na hata sasa kwa wakati huu, ni moja ya biashara kubwa za 2025. Ngoja tuone..mvua inanyesha. Soon tutaona panapovuja
 
Sasa upentekoste asilia ulioingia tanganyika na kuwa na nguvu mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000s umeishia wapi? Maana kuna dhehebu linajiita Nuru ya Jioni, hawa wamejitenga na wapentekoste wa sasa wanaona wamepotea na Mungu hayupo nao. Wana nabii wao wanayemheshimu sana anaitwa Wiliam Branham, ni mzungu mmarekani. Hawa nuru ya jioni wanawapinga sana wapentekoste, wanamtangaza nabii wao kuwa ndiye nabii wa nyakati za mwisho
 
Mbona rahisi tu...Kwa wa Pentecoste mara nyingi Hawa entertain Ile organization ya mtu Mmoja kuwa juu ya wengine so wanatengeneza diversity lakini iliyokuwa coordinated...Wakati makanisa ya litrujia kama RC, KKKT, Anglican Yana organization yenye Mkuu ambaye anaweza ku decide Kwa makanisa yao yote wa Pentecostal haiwezekani, wao makanisa yao ya mahali pamoja yapo na autonomy kubwa lakini wanakuwa na msingi ambao ni common Kwa makanisa yote.

Ukifuata mfano RC unakuta labda Kanisa la St. Peters ndiyo Kanisa haiwezi kupokea amri kutoka Kwa Papa japo Papa au askofu anaweza kuwa ni coordinator kuwaleta pamoja katika mambo ya msingi...

Hii ilifanywa kusudi Ili kuwe na counter balance kwenye power and control ya Imani...Mfano hatari iliyopo Kwa RC ni mfano Papa amekuwa recruited kwenye cult inamaana RC Dunia nzima wanaingizwa bila kupinga kwakua wao Kila kitakachosemwa na Papa ni Yes and Amen...Kwa Pentecost hii siyo possible maana Kanisa au huduma inaweza kukataa na kujitenga na hiyo coordination likajisajili kirahisi ki vyake.

Kwa mfano huo huo Kuna makanisa mengi ya Calvary Assemblies of God hayaamini katika kukata keki, kuuza mchanga na maji lakini Bado ni CAG sawa sawa na Arise and Shine. Wala Askofu Mkuu hawezi kuingilia huduma ya Arise and Shine kwamfano, isipokuwa kumshauri mwenye huduma hiyo na kuendelea kumwombea, akizidisha sana wanamtenga. Anaweza fundisha Somo kama Hilo la kuonya kwenye Mkutano Mkuu wa Kanisa lenyewe la CAG.

Kwa uchache nafahamu Askofu Mkuu wa CAG na mwanzilishi mwenzake ambaye ni marehemu (Bishop Zefania Ryoba) ni watu wenye hekima sana, hata kama hawaamini kitu huwa siyo judgemental lakini hawaachi kuonya Kwa ustaarabu. Kwa kipekee Askofu Mkuu wa CAG Yupo simple sana lakini deep rooted kwenye Imani. I used to doubt him lakini baada ya kumfuatilia niligundua ana moyo wa kichungaji, he gives it time na ameweza kuliweka Kanisa nje ya politics Kwa muda mrefu sana...Ila Sasa wanapoanza kuacha Ile misingi ya awali ataanza kuharibu Imani na kujikuta anaingiia kwenye manipulation ambazo aliweza kukaa nazo kando Kwa muda wote tangu walipianzisha huduma hadi kufanikiwa kujenga taasisi imara yenye wasomi wengi huku akiendelea kushirikiana na Kila mwenye Imani na ideology yake pasipo kujifungamanisha nao.

Pamoja na yote hayo, hata hivyo hutaisikia CAG katika mambo yakutangaza miujiza wala kuchangamana na siasa, this is the first experience namwombea tu Askofu Mkuu wa CAG awe makini sana asijepoteza credibility yake aliyoijenga Kwa muda mrefu. Yeye mwenyewe alivyokuwa powerful kama angekuwa mtu asiyejengwa kwenye misingi imara ya imani angekuwa maarufu sana huku Tanzania na tajiri sana sana, lakini ni mtu wakujizuia sana, lakini si mnyonge, anaijua nafasi yake katika Kristo na huduma aliyopewa kuionhoza ya CAG. Imagine watoto wake wa kiroho wengi ni maarufu sana including huyu wa hiyo huduma na wengine wengi wenye makanisa imara lakini na maarufu sana...wengi wa CAG origional hawajajitangazi ki binafsi na wanafanya kazi ya Mungu Kwa uaminifu wote.
Nimejifunza jambo
 
Back
Top Bottom