Nawaelewa Wapentekoste/Walokole wanapofurahia kuketi moja meza na wakuu. Free Pentecost

Kuna kitu kikubwa sana umechanganya, hapa nitakuelewesha.

Ulokole wa zamani, kwa sehemu kubwa umekufa na kufifia. Mengi ya haya makanisa ya kilokole yanayochipuka sasa yako kibagani, hayana kabisa ile sense ya upentekoste, yamekaa kitapeli na kiuganga uganga. Haya yako tayari kukaa na yoyote ili kulinda utapeli wao. Yanatumia mwamvuli wa upontekoste ili kuficha yanayoendelea nyuma ya pazia.

Lengo halisi la upentekoste halisi tangu ulipoingia Tanzania hapo zamani ilikuwa ni kutengeneza waumini halisi wa kikristo kutoka kwenye mifumo ya kibagani na kidini. Lengo lile taratibu lilianza kubadilika na kuwa, kuvuna waumini kutoka angle yoyote ili kujijenga binafsi kwa maslahi ya sadaka.
 
Ulokole ndio huo huo, sema kulitokea mabadiliko makubwa mbalimbali na ya kasi katika sehemu kubwa ya mfumo wake ikiwemo mavazi, muziki na namna ya waumini wake kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii, siasa na uchumi. Lakini pia mabadiliko makubwa yamewezekana ndani ya ulokole kwa sababu hauko centralised kama makanisa traditional ya RC, KKKT na Anglican
 

Hii combination ya sasa sio ya wapentekoste wote. Kumbuka wale wanaopigwa pale Ubungo nao ni wapentekoste. Hawa wana makundi yanaibuka kila uchao. Na kwa sababu hiyo, hata organisation yake imekuwa ngumu mno. Kila anayepata upenyo, anautumia ipasavyo.

Tofauti na nguli wao. Wako very organised. Na hata sasa wapo ndani kabisa wanaangalia na wanajua kila kinachoendelea.

Kukaa kwao pembeni ni moja ya strategy kubwa za kivita, na zinawaumiza sana baadhi ya watu. Maana wanajua fika, usimchezee simba aliyelala ukadhani ni dume la nyani.
 

Na hata sasa kwa wakati huu, ni moja ya biashara kubwa za 2025. Ngoja tuone..mvua inanyesha. Soon tutaona panapovuja
 
Sasa upentekoste asilia ulioingia tanganyika na kuwa na nguvu mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000s umeishia wapi? Maana kuna dhehebu linajiita Nuru ya Jioni, hawa wamejitenga na wapentekoste wa sasa wanaona wamepotea na Mungu hayupo nao. Wana nabii wao wanayemheshimu sana anaitwa Wiliam Branham, ni mzungu mmarekani. Hawa nuru ya jioni wanawapinga sana wapentekoste, wanamtangaza nabii wao kuwa ndiye nabii wa nyakati za mwisho
 
Nimejifunza jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…