Nawahurumia sana waziri wa afya Ummy Mwalimu na waziri wa Sukari Innocent Bashungwa kwa sababu huu ni mwaka wa uchaguzi!

Nawahurumia sana waziri wa afya Ummy Mwalimu na waziri wa Sukari Innocent Bashungwa kwa sababu huu ni mwaka wa uchaguzi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Unaweza usielewe sasa lakini huko mbele ya safari utaelewa tu, hawa mawaziri wawili wamekalia kuti kavu.

Katikati ya Corona sukari imeadimika madukani watu wanalazimika kusongamana bila kupenda wakiitafuta sukari.

Sisi tulioishi wakati wa vita vya Kagera tunaamini Corona ni vita na hali ya upatikanaji wa sukari haitarejea kwenye hali yake ya kawaida hivi karibuni hivyo waziri awe muwazi mapema wananchi watamuelewa.

Tusisahau kuwa wanasiasa wa Tanzania huangushwa na sukari mfano Prof Mbilinyi, rip Idd Simba nk

Maendeleo hayana vyama!
 
Acha porojo wewe sukari yakufidishia inatoka nje,nje penyewe ndo hivyo sasa hapo waziri ana kosa gani?
 
Bwashee Baraza la Mwaziri si inavunjwa wiki 2 zijazo? Kuti kavu ya nini? Hivi mtu kama Bashungwa anaweza kuwa waziri wa kitu gani? Nimewaza tu. Too naive!
 
Shida ya sukari vipi jamaa hapo shiatle hajasikia? Kufuturu imekuwa shida. maguuuuu geuka Huku uone! Wanatupiga! Sukari wameficha?
 
Leo asubuh baada ya kuambiwa kuwa ule mzigo kutoka Madagascar ni takataka alitoa machozi.
Huyu Mzee wenu hajui namna gani atawambia wananchi juu ya dawa yake pia hata nchi ya Madagascar nao wanasubiri jibu kutoka kwetu kama dawa Yao iko poa ama la!!!

Bwana jiwe amejiweka Kwenye mtego wa mamba mwenyewe kila upande unamsubiri yeye kuanzia Madagascar, WHO, WANANCHI na mawaziri
 
Shida ya sukari vipi jamaa hapo shiatle hajasikia? Kufuturu imekuwa shida. maguuuuu geuka Huku uone! Wanatupiga! Sukari wameficha?
Huwa anakawia sana kusikia shida zenu maana hazimhusu.Yeye ni viwanda ,kazi,ujenzi na kutengua/teua.Hayo mengine hayamhusu unless kama waliosababisha ni mabeberu au mawakala wao(wapinzani esp.CDM) VINGINEVYO HAUTAMSIKIA AKILIONGELEA.
 
anawavutia pumzi. Huyo Waziri asked Mkoa mzuri, maana hali si Hali na hatumsikia anasima nini! Magu akimaliza kujifukiza tu ataweka sawa namuaminia
 
Back
Top Bottom