Nawakumbusha tu: Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake

Nawakumbusha tu: Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
X \ Adventure-360 على X: Nawakumbusha tu Tickets zinakatiwa ofisin jaman  epuka matapeli. https://t.co/g3DYmWVSgh



NAWAKUMBUSHA TU
1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

2. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI"
.
🚶
🚶
🚶
🚶
🚶
🚶

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake
Nawakumbusha tu
🏃🏾


No photo description available.



View:
 

Attachments

  • NAWAKUMBUSHA TU.jpg
    NAWAKUMBUSHA TU.jpg
    26.4 KB · Views: 7
View attachment 2769079
NAWAKUMBUSHA TU
1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

2. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI"
.
🚶
🚶
🚶
🚶
🚶
🚶

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake
Nawakumbusha tu
🏃🏾
Ila huyu Mzee alikuwa jau sana, ukiangalia ubeti wa nne Mzee anajinadi anakufa maskini Hana Mali, sasa Kwa Nini enzi za Uhai wake hakuenda huko shambani kulima Ili apate mali🤦?
 
View attachment 2769079
NAWAKUMBUSHA TU
1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

2. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI"
.
[emoji124]
[emoji124]
[emoji124]
[emoji124]
[emoji124]
[emoji124]

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake
Nawakumbusha tu
[emoji1493]
Nilipofika mjini nadhani nilikosea!
Nikaingia kundini watu nisiowajua!
Wakanikalisha chini elimu kunipatia!
Sina wakumulaumu nadhani nilikosea.

Dah! Haya Mashahiri Nadhani Kipindi Iko Tulikuwa Tunayachukulia Kama Nyimbo Tu Za Kuburudika Ile Leo Yanaishi Na Tunayakumbuka. Sijajua Watoto Wa Siku Izi Uko Mashuleni Ikiwa Haya Bado Wanajifunza Ama La!. Miaka Inaenda Mbio Sana.
 
dah naona nimejichanganya title kidogo. Ila content zinaendana
Inawezekana upo sahihi, kwani baadaye, vitabu vikawa vinatumika tofauti, kati ya shule na shule, tofauti na huko nyuma, ambako, Nchi nzima, shule zote zilikuwa zinatumia vitabu vya aina moja!
 
Mtoto wa kariakoo ukimwambia hizi mambo hawezi kukuelewa..
 
Back
Top Bottom