Nawakumbusha Yanga kuhusu wapinzani wao USM Alger na Mechi zao za nyumbani

magode

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2014
Posts
2,204
Reaction score
3,336
Wakuu,

Umofia kwenu. Binadamu tumeumbwa kusahau. Nimeamua niwakumbushe utopolo aina ya mpinzani waliyenaye akiwa nyumbani. Kwenye mechi za makundi. Mechi ya Kwanza alicheza na Saint Etoil De Lupopo akashinda goli 3-0.

Mechi ya pili nyumbani alicheza Malumo Gallants, akashinda goli 2-0. Mechi ya tatu alicheza na Al Akhdar akashinda goli 4-1.

Kwenye Robo fainali, alicheza na As Far Rabat akashinda 2-0. Nusu fainali akacheza na Asec Mimosas akashinda 2-0. Hizo ni mechi 5 alizocheza nyumbani ameshinda zote, na ameruhusu goli moja tu huku yeye akifunga magoli 13.

Kumbuka yeye kuanzia ngazi ya makundi alikuwa hajashinda mechi yoyote ugenini, mechi pekee aliyoshinda ugenini ni hii aliyomfunga Utopolo. Naamini siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
 
Tukukumbushe na wewe

Yanga tangu ameanza mpaka hapo alipofikia ni mechi Moja tu ndio amefungwa nyumbani.

Kwa hiyo hamna Cha ajabu hapo ,hata huyo USM anaweza kufungwa kwake
 
Mchuzi wa Mbwa hunywewa wa Moto Moto
 
Wakuu,

Umofia kwenu. Binadamu tumeumbwa kusahau. Nimeamua niwakumbushe utopolo aina ya mpinzani waliyenaye akiwa nyumbani. Kwenye mechi za makundi. Mechi ya Kwanza alicheza na Saint Etoil De Lupopo akashinda goli 3-0...
Kwenye mpira lolote linaweza kutokea, mbona hao USM Alger walishindwa kufurukuta nyumbani kw Marumo na kukandwa goli mbili kwa sifuri, lakini Yanga kamkanda Marumo nyumbani kwao. Mpira ni mchezo wa kujipanga kimbinu, ufundi, kutumia nafasi na kutofanya makosa.
 
Tukukumbushe na ww
Yanga tangu ameanza mpaka hapo alipofikia ni mechi Moja tu ndio amefungwa nyumbani
Kwa hiyo hamna Cha ajabu hapo ,hata huyo USM anaweza kufungwa kwake
Yanga alitoa sare na livers, amefungwa na usm Alger. Usm Alger hajafungwa Wala kutoa sare nyumbani. Na siyo kushinda tu, mechi zote kashinda zaidi ya goli moja. Ana wastan wa kushinda magoli 2.5.
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu akaamini yanga anaweza kuja na kombe.

Mechi ya Final CAF kwanini hawakuja na kombe Kwa Mkapa hata kwa Dakika????

CAF WANAFELI SANA
 
Wakuu,

Umofia kwenu. Binadamu tumeumbwa kusahau. Nimeamua niwakumbushe utopolo aina ya mpinzani waliyenaye akiwa nyumbani. Kwenye mechi za makundi. Mechi ya Kwanza alicheza na Saint Etoil De Lupopo akashinda goli 3-0...
Unajitafitia matusi toka kwa gongowazi wewe
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu akaamini yanga anaweza kuja na kombe.

Mechi ya Final CAF kwanini hawakuja na kombe Kwa Mkapa hata kwa Dakika????

CAF WANAFELI SANA
Kombe linakuwepo katika mechi ya mwisho pekee, kombe halizungushwi kila inapochezwa mechi. Mechi ya marudiano ndio fainali yenyewe na ndio kombe litakuwepo uwanjani kwaajili ya timu inatokayofanya vizuri kwa matokeo ya jumla.
 
Kwani haikuwa Fainali.

Just lipitishwe hata kwa Dakika
Lipitishwe ili iweje? Kwani ulisikia ni kombe la maonesho lile? Kwani fainali unaitafsiri vipi? Fainali maanake ni hatua ya mwisho wa mashindano na kutokana na taratibu zilizowekwa hatua ya mwisho kitakuwa na mechi mbili, sasa unawekaje kombe katika mechi ya kwanza? Haijawahi kuwa hivyo
 
Hawa mbumbumbu hawana akili anadhani kombe ni kama mwenge
 
Kazi ya rekodi ni kuvunjwa, USM Alger wamevunja rekodi ya Yanga kwa Mkapa sasa ni zamu ya Yanga kuvunja rekodi kwao na kubeba kombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…