Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda, ameweka wazi kuwa kipindi alichopitia kimekuwa kigumu sana maishani mwake, lakini imani yake kwa Mungu imemsaidia kuvuka changamoto hizo.
Akizungumza jana kwenye misa ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan na kumkumbuka baba mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa, iliyofanyika katika mtaa wa Nyakabindi, mjini Bariadi, Dkt. Nawanda alisema kuwa Mungu huwapa watu mitihani wanayoweza kuivumilia na kupambana nayo.
"Nimepitia kipindi kigumu sana, lakini Mungu humpatia mtu mtihani ambao anajua anaweza kuushinda. Leo, kwa nguvu za Mungu, naweza kusema nimefanikiwa kushinda," alisema Dkt. Nawanda.
Katika hotuba yake, Dkt. Nawanda alieleza kuwa kipindi cha kesi yake kilimfundisha thamani ya kuishi vizuri na watu. Pia alitoa shukrani za dhati kwa wananchi wa Simiyu, akisema kuwa walionyesha mapenzi makubwa na walimuombea kwa bidii.
Soma Pia: Aliyekuwa RC wa Simiyu, Dkt Nawanda ashinda kesi ya “kumlawiti Mwanafunzi”, asema anamuachia Mungu
Ikumbukwe kuwa, mnamo Novemba 20, 2024, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu ilimwachia huru Dkt. Nawanda baada ya kutomkuta na hatia katika kesi ya kulawiti iliyokuwa inamkabili.
Katika misa hiyo, alitoa wito kwa kila mtu kuendelea kumtumainia Mungu, akisisitiza kuwa changamoto za maisha zinapita kwa nguvu za imani na msaada wa jamii.