Liutenant
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 590
- 899
Mwaka 2013 nilikuwa namkubali sana Magufuli kwa namna alivyokuwa anasimama imara kufuata sheria kama waziri. Nilileta huu uzi kumfanyia lobbying kwenye chama Kwa timu hii ya rais na makamu wa rais, CCM tutashinda 2015.
Niliamini huyo ndio atakuwa msaada katika kuijenga Tanzania inayofuata sheria hivyo siku moja nilikutana na Mkapa nikawa namsifia sana huyo waziri. Najua Mkapa alikuwa anampenda Magufuli kama kijana wake lakini watu tulipokuwa tunamtaja mbele yake akapata hamasa sana kumpigania apitishwe.
Bahati mbaya Magufuli alipopata uraisi alibadilika sana na kuacha kufuata sheria na katiba. Hakutaka uhuru wa habari wala changamoto yoyote ya kimawazo. Aligeuka kuwa katili na msema hovyo. Aligeuka akawa muongo sana, aliendesha nchi kwa mikopo lakini anadanganya ni fedha za ndani. Aliua uwekezaji.
Wote tulibaki mdomo wazi kwa aliyoyafanya. Watanzania naomba mnisamehe.