Msingi wa soka ni timu za vijana Malinzi kajitahidi sana kwa hili kukuza na kuweka misingi mizuri kwa soka la vijana na matokeo yake hayataonekana kwa muda mfupi huu,soka la wanawake kajitaidi mpaka kulifufua hili ambalo lilikuwa lishakufa,timu ya Taifa kajitahidi kila awezalo ikiwa ni pamoja na kuleta makocha wa nje na ndani,kugharamia kambi ya timu nje na ndani pamoja kutoa posho stahiki ambapo jambo hili huko nyuma lilikuwa na mshike mshike mpaka bakuli litembezwe. Pia amejitahidi sana kupunguza migogoro ya vilabu na vyama vya soka mikoani ikiwemo TTF yenyewe. Ligi kuu kuonyeshwa live,kutafuta wadhamini kila kona kusaidia vilabu na timu ya Taifa. Kufanikiwa kutupatia nafasi ya kuwa mwenyeji wa u17, kufanya maboresho mbalimbali ya ligi na baadhi ya viwanja. Hayo ni machache tuu yapo mengi.
Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using
JamiiForums mobile app