Nawaonya vijana wa leo mnaofungua makanisa kila kukicha acheni mara moja kama hamna wito, Injili sio biashara.

Nawaonya vijana wa leo mnaofungua makanisa kila kukicha acheni mara moja kama hamna wito, Injili sio biashara.

Matteo Vargas

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2019
Posts
803
Reaction score
1,329
Naandika Uzi huu moyo wangu ukibubujikwa na machozi.

Kuna vitu vinafanyika kwenye madhabahu mpaka mtu unaogopa, na huhitaji PhD Ili kujua wengi wa hawa leo waliojipa unabii ambao sina hakika hata kama walipitia kwenye vyuo vya biblia wakapikwa wakapikika.

Sio mavazi wanayovaa, si lugha wanazotumia vyote havisadifu Ile injili ya kweli tuliyoachiwa na Bwana wetu Yesu Kristo. Kinachoendelea ni wazi watu wanatumia matatizo ya watu kwa kivuli cha unabii waliojivika kufanya biashara makanisani. Ndipo ule unabii wa neno la kwenye biblia la Hosea 4:6 unatimia kwa kusema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"

Katika kitabu cha Mathayo 7:15; neno la Mungu linasema "Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini ndani ni mbwa-mwitu wakali". Hili halina ubishi wengi wa waanzilishi wa makanisa hii leo hasa vijana hawana wito wa kweli ndani yao na neno la Mungu haliko ndani yao bali wana agenda zao kujipatia fedha. Haiwezekani mtu akiweza tu kuhubiri prosperity gospel au kutoka motivation akawa maarufu na ana jina basi anafungua kanisa.

Ukizikiliza hata mahubiri yao mengi hasa clips mbali mbali kutoka TikTok huoni wanakemea dhambi na kuhubiri wokovu 100%, bali wake base kwenye mahubiri ya mafanikio katika maisha, mahusiano ya kimapenzi inshort wanawapa waumini wao wanachotaka kusikia ni tofauti kabisa na wale wahubiri wa barabarani ambao wao nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe.

Nimeshtushwa zaidi kusikia mtu mmoja anaitwa gudlove eti na yeye ana mpango wa kufungua kanisa lakini ukitizama baadhi ya clip zake huko mitandaoni unaona hawa watu waaleta mzaha na neno la Mungu. Ndipo ninasema vijana kama hamna wito acheni kupotosha watu kisa tu una jina au pesa.

Injili ya 2009 kurudi nyuma VS Injili ya 2010 up to date.

Wengi wa vijana tulionza kujitambua mwishoni mwa miaka ya 90 hadi kufikia 2008/2009 tukipelekwa kwenye mikutano ya Injili na wazazi wetu mfano kwa Egon Falk au Christopher Mwakasege watakubaliana nami kwamba Injili iliyokuwa inahubiriwa kipindi kile ni tofauti na hii unayohubiriwa na hawa vijanawa sasa. Mfano mzuri Christopher Mwakasege bado anaefanya mikutano yake hadi leo.

Sasa angalia utaratibu wa huduma ya Mwakasege na huu utaratibu wa wahubiri wa kisasa, wahubiri wa siku hizi pesa, mafanikio, na mahusiano ndio main topic kwenye mahubiri yao Toba, ubatizo na wokovu wa kweli utausikia kwa nadra sana au usisikie kabisa na inafika muda waumini wanalazimishwa kutoa pesa. Ukisoma 2 Petro 2:3 inasema "Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao Toka zamani haikawii, Wala uvunjifu wao hausinzii" Ndio maana hao wenye makanisa Ili uweze kuwaona lazima utoe pesa hii ni Injili au biashara??

Na wengi wao wana utajiri wa kufuru na wanaishi maisha ya anasa wakati hao waumini wao waliopotea kwa kukosa maarifa wanaishi kwenye ufukara wa kutupa. Kinachoumiza pia kuna nchi nyingine manabii na mitume hao wananajisi madhabahu wa kuwavua nguo waumini wao ama hata kuwashika sehemu zao za siri kwa kigezo cha kufanya maombezi ya uponyaji.

Kama wanayafanya mambo haya hadharani ni nini kinachoendelea huko maofisini mwao wanapojificha eti bila hela huwezi kuwaona?? Na kuna member humu aliwahi kulalamika mke wake anamsikiliza zaidi mchungaji/mtume wake kuliko yeye. (There must a be a problem and mchungaji is a problem)

Na hata kwaya nazo huko makanisani hasa haya kisasa yanayoendelea ni ushetani mtupu yaani leo hii kwaya kucheza Amapiano kanisani sio issue, watu wanakata viuno na viongozi wa kanisa hawakemei wapo kimya mpaka unajiuliza wanaburudika au?? Na mbaya zaidi the so called Praise and worshipping team nguo wanazovaa kuna muda unaogopa wewe unayetazama. Hii ndio Injili aliyosema Yesu katika Marko 16:15 kuwa tuenende ulimwenguni mwote tukaihubiri Injili kwa kila kiumbe?

Lakini pia nilishutuka kuona Pastor Kapola kanisani kwake wanawake wamevaa skin jeans zimechora miili yao guys let's have some respect we can't worship our Almighty God in this way.

Sio wote hawana wito ila wengi wao ukiona tu anachofanya maarifa ya asili yanakataa sababu ni utapeli wa wazi wazi. Mfano Nabii Olivia wa kule Sinza aliwahi kumwambia mtu aliyekuwa anamuombea kuwa apige kelele, haya maigizo ndio yanapaka matope hata wale wenye wito wa kweli.

Vijana wote tunaoifahamu kweli ya Kristo tutumie akili zetu na elimu zetu kukemea utapeli unaofanywa na vijana wenzetu kisa tu wapate utajiri wa haraka kwa staged miracles. Hii haikubaliki na MUNGU HADHIHAKIWI.
 
Jamaa zangu wengi baada ya ajira kusua sua kipind cha JPM waliamua kujiingiza kwenye upastor .

Hata baada ya Samia kuanza kuajir wao hawatak kabisa kuomba na Kwa sasa Wana hela chafu
 
Jamaa zangu wengi baada ya ajira kusua sua kipind cha JPM waliamua kujiingiza kwenye upastor .

Hata baada ya Samia kuanza kuajir wao hawatak kabisa kuomba na Kwa sasa Wana hela chafu
Hii ni hatari sana kufanya kazi usiyokuwa na wito nayo na kuna vijana wengi pia wana ndoto za kufungua makanisa watajirike
 
Haijalishi hata kama ni manabii wa uongo lakini wanawaleta watu kwa Kristo wakishaujua ukweli wanaenda kutafuta watumishi wa kweli wa Mungu
 
Haya mambo yasingetokea kama ilivyotabiriwa basi Biblia ingeonekana ni kitabu cha uongo acheni magugu na ngano vimee pamoja hadi wakati wake
 
Unawaonea bure .

Shida ni waumin wa dini ya kikristo
Mbona vijana wa kiislam hawafungui misikit wala kujiita masheikh?

Niny wenyew mmeifanya kazi ya Mungu NI kazi Kama kazi nyingine na si huduma.
 
Pana motivation speakers na pana mens of God ipo haja ya mamlaka kuwakategorize.
Mfano kiboko ya wachawi yeye kabase kuuwa wachawi so ni wewe tu unachagua unataka injili kavu za kina mbarikiwa, Cassian,mwangila au unataka zile za kupokea makontena
 
Back
Top Bottom