Nawapiga chini marafiki wote wasiokuwa na tija kwangu

Nawapiga chini marafiki wote wasiokuwa na tija kwangu

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Yeyote anayekunyima furaha, piga chini.

Maisha haya ni mafupi, haijalishi utaishi miaka 100 au 200; bado tutasema maisha ni mafupi tu, ikiwa na maana hapa duniani tunapita.

Hakuna haja ya kuwa na ndugu, marafiki, wachumba n.k wasiojielewa, ambao wanakupa msongo wa mawazo muda wote, na kukunyima furaha katika maisha yako.

Anayekupa muda mwingi kuumiza kichwa huku ukimuwaza yeye tu, na kupoteza furaha uliyonayo; wakati mwingine anakuletea magonjwa ya moyo, kisukari n.k katika kumfikiria.

Huu ni muda muafaka wa kumpiga chini; na kuambatana na ndugu, jamaa, wachumba, marafiki wapya n.k watakao kupa furaha na kuona dunia ni sehemu sahihi ya kuishi.

Wakuu, naanza kupiga chini vibwengo wote.
 
Mshikaji gani nikikosa mwana nikipata unavunja
Nikizipata unataka ule nao ila zenu mnavunga
Sio mwanangu nishakudelete
Nishajua kuwa we snitch
Unamkuwadia dem wangu vipi?
Kigegu unakataa kulipa

Kama rafiki humwelewi, mpunguze
Kuropoka ropoka hachelewi, mpunguze
Ukimuona sio, mpunguze
Anapenda mademu wa wenzio, mpunguze
Anapenda bata hana kazi, mpunguze
Rafiki gani huyu dwanzi, mpunguze
Rafiki gani kwenye raha, mpunguze
Kwenye shida mbali anakaa, mpunguze
 
Yeah kuna tofauti ya mwana na rafiki yeah
Mwana wa wsaliti, mwana anaweza kuwa mcheshi kumbe ni mnafiki
Mwana akipata kidogo anajiona pipi
Mwana haambiliki sasa huyu ni mwana au ni kiti
 
Nakumbuka kuna kipindi pesa yangu ilikuwa nje nje tu full bata na ndugu na jamii baadae kushtuka nikawa nainvest sehemu ndugu na jamii yote ikanitenga nikabakia na familia yangu tu kila mtu akawa ananiona nuksi ila kwangu lilikuwa Somo zuri nikawapiga chini mmoja mmoja mpka ndugu bila kujali nikadeal na wale tu ambao tulikuwa pamoja kwenye majanga sasa nashukuru Mungu mambo yameanza kukaa sawa sijui wanapeana taarifa kila mtu anajaribu kutengeneza tena urafiki na mie ila nikimjua tu anakula tofali maana hana faida na Mimi ila yeye ndio mnufaka na Mimi
 
Yeah kuna tofauti ya mwana na rafiki yeah
Mwana wa wsaliti, mwana anaweza kuwa mcheshi kumbe ni mnafiki
Mwana akipata kidogo anajiona pipi
Mwana haambiliki sasa huyu ni mwana au ni kiti
Ni kusafisha kitabu mkuu, asiyekuwa na tija weka pembeni
 
Mshikaji gani nikikosa mwana nikipata unavunja
Nikizipata unataka ule nao ila zenu mnavunga
Sio mwanangu nishakudelete
Nishajua kuwa we snitch
Unamkuwadia dem wangu vipi?
Kigegu unakataa kulipa

Kama rafiki humwelewi, mpunguze
Kuropoka ropoka hachelewi, mpunguze
Ukimuona sio, mpunguze
Anapenda mademu wa wenzio, mpunguze
Anapenda bata hana kazi, mpunguze
Rafiki gani huyu dwanzi, mpunguze
Rafiki gani kwenye raha, mpunguze
Kwenye shida mbali anakaa, mpunguze
Ni kufanya maamuzi magumu tu mkuu
 
Back
Top Bottom