Nawapongeza LATRA na SUMATRA kwa kuruhusu mabasi kusafiri saa 24

Bongo bana..yani mtu anapongezwa kwa kutimiza wajibu wake?no wonder miviongozi inajiona Mungu...
 
Life is all about risks.. ukiona mwanaume anahofia kurisk jua kuna shida mahali
Usiku kwangu ni salama zaidi kuliko mchana leo nchi nzima ok nafurahia usafiri huo ambao ulianzia Kwa wizi wizi mbeya uyole ilikua inaitwa hakuna kulala ikiwa ni Noah old, mnatembea usiku kucha asubuhi mjini unafanya mambo yako jioni unarudi, au unavizia IT alfajiri uko mbeya, tunduma au kyela, hivo wafanyabiashara wakawa wanapambana, ikatoka baadae Kilimanjaro na Arusha nao kiwiziwizi ukiacha magari ya magazeti wao wakaanza na coaster watu wakapambana sana , coaster zikatapakaa mwanza, kahama, Moshi, mbeya, zikapigwa marufuku kifika Dar, watu ikabidi kuomba vibali vya msiba mnaweka picha ya maua mbele ili mtoboe mkiulizwa mwili uko wapi mnasema ndio tunaufuata dar, wakati mnarudi mnasema mwili umetangulia sisi ni familia moja tunaenda msibani issue ikastukiwa zikapigwa burn, ikawa sasa mnaletwa mpaka moro then pale mnajifaulisha kufika mjini, hapo bado hatujasema wale wanaopanda tank za mafuta na malori ya mizigo au kuungaunga bila uhakika,
 
Tusisahau kutoa pongezi kwa Mhe. Tulia na yule mkata kiuno.
 
Hii kitu ni bomba sana... nilikuwa Nyanda za juu kusini, saa 10 jioni nikapata dharula natakiwa kurudi Dar. Nikaingia tu kwenye mtandao, kata ticket, saa 12 niko kwenye basi.

Nilichonotice kwenye ile safari, madereva hata hawakimbii, lakini saa 1 asubuhi tulikuwa Dar, very comfortable
 
Kwa sasa nchi nzima ya wilaya zake uamue wewe tu kulala lakini, magari yako sehemu zote leo hii kahama to Dar ni elfu sitini nauli, hapo barabara nzuri leo watu wa kasulu to dar nauli elfu hamsini, Moshi, Arusha Kwa route yoyote Tanzania unafika muda wowote hivo kwenye mazuri tuyaseme, leo watu wa misiba, biashara hakuna tena presha unapata taarifa mchana unajiandaa usiku kuondoka,
 
Siku hizi gharama za kulala tunazisave.

Ondoka usiku fika asubuhi fanya mishe zako, geuza usiku fika asubuhi endelea na mishe
 
Imagine ungetakiwa uondoke kesho yake alfajiri pasingekuwepo na usafiri wa 24 hrs.

Tukiachana na risks mbalimbali kwenye usafiri, ila huu wa muda wote ni muhimu sana.
 
Nimepanda sana coaster za Dar -Moshi tunaachwa njia panda .

Leo mwanaume anasema ni risk
😏😏
 
Nimepanda sana coaster za Dar -Moshi tunaachwa njia panda .

Leo mwanaume anasema ni risk
😏😏
Usishangae wanawake Kwa sasa wanamiliki uchumi kuliko sisi, tumekua waoga sana, wazee zamani walisafiri na wakiona wanyama wakali wanajificha kwanza au kuwasha moto, binti anajituma kuwahi memorial alfajiri ili afunge makapeti ya mtumba na mashuka ili awahishe mzigo dar au dodoma akimaliza anakamata hakuna kulala hapo miezi ya baridi kafika silari kupokea belo za makoti na blanketi kutoka nairobi, anaunga kwenda chap akafungue mzigo makete,njombe, mafinga, hapo katangulia na gloves na mizura miezi mitatu humuoni kwake yuko barabarani leo umweleze mambo za risk akuelewe kwani karogwa,
 
Pia hii ya 24 imepunguza ajali za barabarani.

Magari yalikua yanashindana ili kuwahi kufika, sasa hiyo haipo tena.

Kikubwa ni kudhibiti mwendo na kuhakikisha barabara zinapitika muda wote pamoja na kuziba mashimo ya barabarani kwa wakati.tu basi.
You're right! Fikiria pale stendi Mbezi au Ubungo zamani yanaachiwa magari 120 at per! Lazima uwendawazimu uwepo kwa baadhi ya madereva hence ajali! But nowadays, kila gari huondoka kwa ratiba yake lenyewe.
 

"na SUMATRA"! Ndiyo sababu hizo pongezi umezitoa leo.​

 
Tizaja sana nguku na kio haja mbwewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…