Hii siku ni ndefu
Na Sasa Bado ni asubuhi, naona baadhi ya viongozi na machawa wakikejeli gen Z kuwa Kiko wapi?
Hii inaweza kuwa aina mojawapo ya uchochezi
Hata sijui hii serikali wanataka nini? Maridhiano au mauaji.
Hali ya utulivu ikirejea mnaanza tambo na kutonesha waathirika?
Kwamba wauaji wanatambia ndugu, wazazi, wake na yatima wa Watanganyika waliokufa, kuwa Kiko wapi tuliwaua na Sasa hata Kuandamana tumewadhibiti
Hizi tambo sio za kuishabikia wala hamna mshindi hapa, wala sio mashindano kuwa polisi au serikali wanashindana na vijana wenye hoja za msingi kama Katiba mpya, kupinga ufisadi na Rushwa.
Kupinga utekaji na mauaji
Kupinga ulaghai kwenye chaguzi
Chungeni kauli zenu
Hii siku ni ndefu mno
Hakuna haja ya kutambia Watanganyika waliopata na madhira
Acha kabisa kutambua
Period