Nawashauri Wasanii maarufu Bongo mjiondoe katika Mtandao wa YouTube, Tengenezeni Platform zenu wenyewe

crankshaft

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,427
Reaction score
3,438
Anzisheni Platform Zenu , Mzitangaze Sana Kwenze Page Zenu Za Social Media .

Tufanye Diamond Utapata Fans Waelewa Hata Milion 2 Katika Fans Wako Karibu Milion 20 Kwa Page Yako Ya Instagram Na Mitandao Kwa Ujumla, kazi Zako Mpya Sasa Unakuwa Unaweka HuKo,
Mfano Kabla Ya Kuachia Ngoma Hata Siku Tatu Kabla Unaposti Pale Insta Page Yako Mashabiki Zako Tunachanga Hata 200/= Tu Ili Kuweza Kupata Kazi Yako. Unaweza Kupiga 400m Ya Haraka.

Ukipata Pesa Nyingi Maana Yake Unaweza Tafuta Namna Bora Zaidi Ya Kusambaza Kazi Zako Kimataifa Na Kuliteka Soko.

Youtube Tuwaachie Wasanii Wanaoibukia Kwa Ajili Ya Kujikuza Zaidi, Ninyi Mmeshapata Umaarufu Na Mashabiki Wa Kutosha Tengenezeni Pesa Kwa Sasa,

Kwa Hapa Bongo Youtube Inawahitaji Kuliko Unavyoihitaji Na Sio Rafiki Kwa Sanaa Yetu.

Tunapenda Kuwaona Wasanii Wetu Wanakuwa Matajiri Kutokana Na Sanaa Zao Na Sio Kuishia Kuwa Maarufu Tu.

Inasikitisha Wasanii Wetu Bongo Wanakaa Kwenye Industry Kwa Muda Mrefu Lakini Hawana Cha Kujivunia Zaidi Ya Umaarufu Wa Insta.
 
Mkuu wabongo wanapenda mtelezo Sana , mi huwa nauza home appliances , kwa kweli napenda kuuza vitu quality, huwa napenda nijiamin napompatia mteja kitu Bora , sema kitu kizur ni mkasi , wabongo wengi huwez wapata , wanapenda mtelezo mwisho wa sku unawaletea tuu low quality ndo unapata hela , Diamond ashajarbu wasafi.com , Ila fitna ikawa nyingi plus wabongo wazee wa mtelezo ikajifia , jamaa akapiga chini
 
Mzee umeongea vitu imaginary,Mtu kashindwa hata share tu ngoma yako,ataweza kukuchangia 200? Sio bongo hii

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app

Hao Watu Watu Wapo Ndo Maana Nimesema Kwa Wachache, Mfano Out Of 8m Alikiba Fans Ndani Ya Instagram Akawa Na Loyal Fans 1m, Hawa Wakanunua Wimbo Wake Kwa 200/=, Huyu Msanii Anatengeneza 200m Ambayo Anaweza Asiipate Kwa Nyimbo Zake Zote Pale Youtube.
 
Mkuu wabongo wanapenda mtelezo Sana , mi huwa nauza home appliances , kwa kweli napenda kuuza vitu quality, huwa napenda nijiamin napompatia mteja kitu Bora , sema kitu kizur ni mkasi , wabongo wengi huwez wapata , wanapenda mtelezo mwisho wa sku unawaletea tuu low quality ndo unapata hela , Diamond ashajarbu wasafi.com , Ila fitna ikawa nyingi plus wabongo wazee wa mtelezo ikajifia , jamaa akapiga chini

Ni Kweli Mkuu Lakini Sio Wote Ndio Maana Hapo Nimeonesha Sehemu Tu Ya Mashabiki.
Shida Ya ile Wasafi.com Ni Kwamba Ilikuwa Inaweka Kazi Lakini Pia Zilikuwa Zinapatikana Youtube Bure.
Kwa Mfumo Ninaopendekeza Mimi Nataka Zisipatikane Youtube Au Zimetikane Baada Hata Ya Mwezi Baada Ya Kuuza.
 
Bongo land hakuna jipya🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mzee umeongea vitu imaginary,Mtu kashindwa hata share tu ngoma yako,ataweza kukuchangia 200? Sio bongo hii

Sent from my M2101K7AG using JamiiForums mobile app
Wewe ndo unaongea vitu imaginary.

Muulize mange anapata sh ngp kwenye app yake kwa kuweka scandal za haohao wasanii. Yaan unakuta mtu analipia buku kwenda kuona mchepuko mpya wa mbosso ni nani.

Ni kwamba tu wasanii wetu hawajielewi, watu baki wanapiga hela sana kwa kutumia umaarufu wa haohao wasanii.

Nikupe mfano wa JAY Z, jamaa alipokua unsigned alikua anasambaza muziki wake yy mwenyewe, baadae akapata label ila alipoingia huko akaona hakuna wanachomfanyia ambacho hawezi yeye kujifanyia, na ndipo akatoka akaanzisha Roc-A-Fella and the res is history.

Wanamuziki kama kina harmonize, marioo, diamond etc... wakichukua hio approach kwa upande wa platforms watatoboa sana. Tena mtu kama mondi ndio atapiga hela hata kufikia level za kina didy na jigga
 
Mkuu wabongo wanapenda mtelezo Sana , mi huwa nauza home appliances , kwa kweli napenda kuuza vitu quality, huwa napenda nijiamin napompatia mteja kitu Bora , sema kitu kizur ni mkasi , wabongo wengi huwez wapata , wanapenda mtelezo mwisho wa sku unawaletea tuu low quality ndo unapata hela , Diamond ashajarbu wasafi.com , Ila fitna ikawa nyingi plus wabongo wazee wa mtelezo ikajifia , jamaa akapiga chini
Wasafi.com ilifeli hata kabla ya kuanza, ww unauza mziki ambao upo available pia youtube au boomplay nani atanunua. Ukiwa na business lazima utengeneze demand, limit & control supply thn cheza na wateja wako. Ukiweka mifano ya home appliances ni kufananisha mambo yasofananishika, hivi ushajiuliza kwa nn kwenye macasino wanatumia zile coins badala ya hela halisi? Sababu zile ni rahisi mtu kupuuzia hata akilose, mziki wa mondi akiuza miambili akipiga zake 1M views hata kwa mwezi ni 200M

Kwa sasa kuna technologies kama NFT na blockchains, na hizo zikitumiwa vzr unaweza tengeneza platform moja very efficient kulimit piracy ya kazi za wasanii
 
Wewe ndo unaongea vitu imaginary.

Muulize mange anapata sh ngp kwenye app yake kwa kuweka scandal za haohao wasanii. Yaan unakuta mtu analipia buku kwenda kuona mchepuko mpya wa mbosso ni nani.

Ni kwamba tu wasanii wetu hawajielewi, watu baki wanapiga hela sana kwa kutumia umaarufu wa haohao wasanii.

Nikupe mfano wa JAY Z, jamaa alipokua unsigned alikua anasambaza muziki wake yy mwenyewe, baadae akapata label ila alipoingia huko akaona hakuna wanachomfanyia ambacho hawezi yeye kujifanyia, na ndipo akatoka akaanzisha Roc-A-Fella and the res is history.

Wanamuziki kama kina harmonize, marioo, diamond etc... wakichukua hio approach kwa upande wa platforms watatoboa sana. Tena mtu kama mondi ndio atapiga hela hata kufikia level za kina didy na jigga
Wewe unajua hizi mambo kabisa maana nyuzi zenu huwa nakuona. Hilo jambo mnalotaka si rahisi kama mnavyotuaminisha, umemtaja Jay Z nakutajia Soulja Boy alipoanzisha gaming console na ikafa, huyohuyo alikuwa na streaming platform miaka ya kabla ya 2010 na ikafa vilevile. Kwanini kina Drake, Jay Z, Ed Sheeran na wakubwa kama hao wasitengeneze mshindani wa YouTube mje kusema Diamond asiye hata na video ya viewers 100M.

Wabongo wengi hawapendi subscription hivyo itabidi utengeneze pesa kupitia ads. Google walinunua YouTube na wamewekeza hela nyingi. Sasa mpaka uanzishe platform usimame na ufanye marketing, mpaka wateja wajae kufikisha namba za waleta ads. Na bado YouTube ina kila kitu, hii platform itakayoanzishwa Bongo mpaka itafute contents nyingine sio leo, itarajiwe itakuwa inalipa content creators vizuri zaidi.

Kama Wasafi media wasanii wanagawanyika sembuse hiyo platform. Inahitaji investment kubwa ya kusubiri breakeven miaka kadha baadae jambo ambalo wasanii hawataki labda ulete investors wengine.

Ukiachana na Uber na Bolt, platforms za kibongo tunaona zinavyopambana lakini bado. Hata hii ya video au streaming sio rahisi hivyo
 
Wewe unajua hizi mambo kabisa maana nyuzi zenu huwa nakuona. Hilo jambo mnalotaka si rahisi kamaube mje kusema Diamond asiye hata na video ya viewers 100M.

nambitakayoanzishwa Bongo mpaka itafute contents nyingine sio leo, itarajiwe itakuwa inalipa content creators vizuri zaidi.

Nakuona Mzee Wa Masilaha. Anyways Turudi Kwenye Mada. Hauwezi Kulinganisha Dunia Ya 2010 Na Sasa.
Hawa Akina Drake Hawana Haja Ya Kushindana Na Youtube Kwa Sababu Inawalipa Vizuri Wana Fans Worldwide.
Diamond Anaweza Kutumia Hii Strategy Kwa Local Loyal Fans.
Ni Kweli Wabongo Hawapendi Subcription Lakini Sio Wote Bado Wengi Ni Waelewa Ndio Maana Nimetoa Mfano Hapo Kwa Small Portion Ya Diamond Fans Out Of 17m Fans Wa Instagram,wakalipa 1m Kwa 200/=.
Haihitaji Content Nyingine Zaidi Ya Kazi Zao Labda Zaidi Habari Zao.
Youtube Sio Mtandao Rafiki Kwa Wasanii Wetu Wa Bongo,wanatumia Gharama Kubwa Kuandaa Kazi Ila Haulipi Zaidi Ya Umaarufu Tu.
 
Hizo silaha nimepumzika kuzisema kwa sasa naongeza content. Soulja Boy ana miaka 32 huwezi sema dunia yake sio ya sasa kaanza imba ana kitu kama 17 au 19 years.

Kinachofanya YouTube isilipe vizuri kwa wabongo ni umaskini wetu, hata blog views za ads hulipa vizuri kwa North American views Ila kidogo kwa African views. Kinachowafanya wasanii wetu wasiwe na hela ni njaa kali ya mashabiki wao ambao ni sisi.

Spotify inalalamikiwa mara zote kuwalipa kidogo wasanii na Drake juzi juzi hapo aliwashauri waongeze. Sio wabongo tu wanaonuonywa.
Kwanza algorithm ya kulipa msanii hizi streaming platforms ni ngumu kueleweka na siri kimakusudi.

YouTube ni platform ya kutafuta kujulikana zaidi wala sio kutengeneza hela uko, kujulikana kwenyewe kunaleta hela baadae. Nadhani ushajua kwanini Rihanna hakulipwa kwenye Super Bowl, wala hakuna msanii anayelipwa uko tena wengine kama Ed Sheeran na J Cole walitoa hela zao mfukoni kuongezea kuandaa show.

Androids zinakuja na YouTube na Google search engine kwa sababu. Ili utoe upinzani ujipange na budget kubwa mno. Uber tangu ianze hadi leo imetengeneza faida mwaka 2018 tu baada ya kuuza segment yake mojawapo ya biashara. Miaka mingine ni hasara ya $ billions, sasa ukija hapa ukadai eti wabongo watapiga hela kirahisi kwenye ride services ntakushangaa.
Google iliinunua YouTube kwa $ 1.6 billion mwaka 2006 ila mwaka jana tu YT iliingiza faida ya $ 29 billion. Sasa ukiwauliza wamewekeza kiasi gani humo pamoja na supporting model yao utajua sio kazi ndogo.

Hakuna msanii bongo utamwambia wekeza hapa upate faida 10 yrs later akuelewe. Washindwe clothing lines nyepesi kama Vunjabei (ni biashara nyepesi sana kama mtu asiyejua misimu yote lini timu inatakiwa ivae jezi anaiweza hata kilaza ukimpa hela anaifanya) waje waweze biashara ngumu hivyo.
 
Mkuu wabongo wanapenda mtelezo Sana , mi huwa nauza home appliances , kwa kweli napenda kuuza vitu quality, huwa napenda nijiamin napompatia mteja kitu Bora , sema kitu kizur ni mkasi , wabongo wengi huwez wapata , wanapenda mtelezo mwisho wa sku unawaletea tuu low quality ndo unapata hela , Diamond ashajarbu wasafi.com , Ila fitna ikawa nyingi plus wabongo wazee wa mtelezo ikajifia , jamaa akapiga chini
Hao wasanii wenu huwa wanarudisha nini kwa jamii,au ndy mnawakamua kwa matamasha yenu kwa viingilio
Mnataka nyie tu ndiyo mpate

Ova
 
Anzisheni Platform Zenu , Mzitangaze Sana Kwenze Page Zenu Za Social Media .

Tufanye Diamond Utapata Fans Waelewa Hata Milion 2 Katika Fans Wako Karibu Milion 20 Kwa Page Yako Ya Instagram Na Mitandao Kwa Ujumla, kazi Zako Mpya Sasa Unakuwa Unaweka HuKo,
Mfano Kabla Ya Kuachia Ngoma Hata Siku Tatu Kabla Unaposti Pale Insta Page Yako Mashabiki Zako Tunachanga Hata 200/= Tu Ili Kuweza Kupata Kazi Yako. Unaweza Kupiga 400m Ya Haraka.

Ukipata Pesa Nyingi Maana Yake Unaweza Tafuta Namna Bora Zaidi Ya Kusambaza Kazi Zako Kimataifa Na Kuliteka Soko.

Youtube Tuwaachie Wasanii Wanaoibukia Kwa Ajili Ya Kujikuza Zaidi, Ninyi Mmeshapata Umaarufu Na Mashabiki Wa Kutosha Tengenezeni Pesa Kwa Sasa,

Kwa Hapa Bongo Youtube Inawahitaji Kuliko Unavyoihitaji Na Sio Rafiki Kwa Sanaa Yetu.

Tunapenda Kuwaona Wasanii Wetu Wanakuwa Matajiri Kutokana Na Sanaa Zao Na Sio Kuishia Kuwa Maarufu Tu.

Inasikitisha Wasanii Wetu Bongo Wanakaa Kwenye Industry Kwa Muda Mrefu Lakini Hawana Cha Kujivunia Zaidi Ya Umaarufu Wa Insta.
Sidhani kama YT inawahitaji kuliko inavyowahitaji.
Halafu wabongo wagumu nunua kazi ndio maana ile platform ya diamond ya kuuza nyimbo haikuchukua hata miezi sita ilikiwa ishapotea
 
Wewe unajua hizi mambo kabisa maana nyuzi zenu huwa nakuona. Hilo jambo mnalotaka si rahisi kama mnavyotuaminisha, umemtaja Jay Z nakutajia Soulja Boy alipoanzisha gaming console na ikafa, huyohuyo alikuwa na streaming platform miaka ya kabla ya 2010 na ikafa vilevile. Kwanini kina Drake, Jay Z, Ed Sheeran na wakubwa kama hao wasitengeneze mshindani wa YouTube mje kusema Diamond asiye hata na video ya viewers 100M.

Wabongo wengi hawapendi subscription hivyo itabidi utengeneze pesa kupitia ads. Google walinunua YouTube na wamewekeza hela nyingi. Sasa mpaka uanzishe platform usimame na ufanye marketing, mpaka wateja wajae kufikisha namba za waleta ads. Na bado YouTube ina kila kitu, hii platform itakayoanzishwa Bongo mpaka itafute contents nyingine sio leo, itarajiwe itakuwa inalipa content creators vizuri zaidi.

Kama Wasafi media wasanii wanagawanyika sembuse hiyo platform. Inahitaji investment kubwa ya kusubiri breakeven miaka kadha baadae jambo ambalo wasanii hawataki labda ulete investors wengine.

Ukiachana na Uber na Bolt, platforms za kibongo tunaona zinavyopambana lakini bado. Hata hii ya video au streaming sio rahisi hivyo
Mifano unayotoa bado haipo relevant na situation ya sasa.

Unasemea kina drake, hao platforms zinawalipa, hivi unaposikia drake kafanya mauzo makubwa ya album yake unajua hayo mauzo yamefanyikia wp?

Haya njoo bongo, wasanii wangapi wanatoa albums lkn wanaishia kujisifia kwa kupata streams tu na wala sio mauzo!..

Drake na wasanii wengine wa mambele hawawezi anza kutengeneza platforms from scratch kwa sasa sababu zilizopo zinawalipa vizr.

Huku kwetu wasanii inabidi wajiongeze. Unajua mie nmefanya kazi na startup kama mbili hivi, wanatengeneza ideas ambazo haziko relevant na use cases za kiafrika. Same here.. wasanii wakubwa kama diamond wakiamua kuwekeza wakatafuta wataalam watengeneze platform ambayo ni relevant kwa waafrica mbona kutoboa kunaonekana kabisa... Ushajiuliza mfano huduma kama M-Pesa, hizi hazipo USA, hata wazungu wanatu-appreciate kwa hilo, lkn huku zinatumika kwa sababu ziko relevant na mazingira.

Wabongo tulivyo na akili fupi mtu akisema kutengeneza platform, atatafuta kampuni limtengenezee clone ya youtube au spotify, bila kuangalia nature ya watu anaotaka kuwafikia...

Point yangu ni hawa wasanii wakubwa kukaa chini kushauriana na wataalam then watoke na platform moja ambayo ni relevant kwa wasanii na wasikilizaji wa africa. Hizo insta na youtube watumie kuwavuta mashabiki na ndani ya 2 yrs utashangaa.
 
Back
Top Bottom