T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Mkuu hizo platforms za bongo zinazolipa kidogo ni zipi. Na platforms zote za kimataifa hazina calculation inayojulikana fika ya malipo hata wasanii wenyewe huwa hawajui watalipwaje labda makadirio.kutokana na umaskini wetu utube sio rafiki kwetu.
platform za bongo malipo huwekwa siri kwa sababu ni kidogo.
spotfy, i tunes na apple wanalipa vizuri na malipo yao yapo wazi.
wasanii washakuwa maarufu hawahitaji youtube kujulikana na kwenye soko la kimataifa utube sio njia bora zaidi. Ni lazima auze kazi zake apate pesa nyingi zimsaidie kujitangaza kwa namna bora zaidi.
hatuhitaji kuleta upinzani kwa utube bali platform ya kuuza kazi,uwekezaji wameshaufanya kwenye majina yao.
Msanii kuwa maarufu anahitaji kuzidi kubaki juu au kuendelea. Tena achana na wa mbele uko, hapa kila siku si unaona wanashindana trending in YouTube? Inawasaidia wao kuliko inavyowasaidia uko mambele. Mtu kama Kendrick Lamar akatoa Mr. Morale album akauza copies zake laki kadhaa akakusanya pesa, anasubiri shows, World tour, collaborations, deals kisha asubiri hizo streaming na hela ya mboga ya YT.
Bongo hapa kuna msanii atauza copies mtaani humu? Nani huyo labda Maalim Nash anayefanya delivery mtaani kwake. Vincent Kigosi "Ray" kaanza kuigiza sijaanza shule, last week namuona anakopeshwa milioni 40 alipe ndani ya 2yrs. Hivi msanii mkongwe na star wa Bongo Movie kama yule ni wa kukopeshwa 40M zimsaidie kikazi? Watu walitoa kazi zikaishia kutolewa nakala vibanda umiza.
Sasa uanzishe platform ulipishe watu wa jamii hiyo kweli utegemee ishindane na YouTube.