Nawashauri Wasanii maarufu Bongo mjiondoe katika Mtandao wa YouTube, Tengenezeni Platform zenu wenyewe

Nyie ndo wale ambao mmeshindwa youtube na mond kawaacha mbali sana

Kujufunza kwa aliyefanikiwa ni jambo jema

Dunia ni kijiji usiwatenge wasanii wa tz a dunia
 
Ni Kweli Wabongo Hawapendi Subcription
Af hii sio kweli.

Mbona kuna app za bongo zinatumia subscription based na wanapiga mpunga mzr tu. Kinacho-matter ni idea yako tu, tengeneza kitu relevant wateja utawapata.
 
Wazo ni zuri ila sasa utekelezaji wake ni ghali sana kulingana na tabia ya watumiaji wa bidhaa na huduma za wasanii wetu, uuzaji holela wa kazi za wasanii bado ni mwiba mkali yani mambo ni mengi mkuu.
 
I second your thoughts.
Nimewahi kitu kama hiki na nika draft concept paper. Sikupata uungwaji mkono. Nikapotezea. Ilikua back then 2012.
 
Unamtolea mfano Jay Z ambae yupo kwenye nchi ambayo hakuna site za kuweka KAZI za wasanii bure na watu wakadownload bure.

Tanzania ukiachilia mbali hiyo YouTube kuna website lukuki zinafanya piracy ya kuweka nyimbo na KAZI za wasanii.


Marekani huwezi kukuta vibanda mitaani vinauza KAZI za wasanii kwenye flash. Tanzania nzima kuna vibanda watu wanauza na kuwawekea watu nyimbo kwenye flash Kwa bei nafuu.


Mazingira ya ulinzi WA Kazi za wasanii Kwa hizi nchi mbili ambazo unatolea mfano ni tofauti kabisa. Kwa Marekani ni rahisi Sana msanii kusimamia KAZI yake Kwasababu nchi ya Marekani inalinda KAZI za wasanii Kwa nguvu zote. Marekani huwez kukutana na site kama za wakina DJ MWANGA.


Hivyo basi Kwa hicho ulichosema na unataka kushauri hapa hakuna msanii atakaefanikiwa hata robo.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Acheni kudanganya hapa Kwa tanzania bado Sana kwenye issue ya kulinda KAZI za wasanii.

Kuna wasanii wengi hapa hapa tanzania wamejaribu hizi njia Ila wamefeli.


Wasanii WA tanzania wajibrand wapate endorsement kubwa. Huwezi Kutegemea utajiri wa msanii utokane na nyimbo Tu anazofanya. Nenda hata US wasanii wote mabilionea hawajawa mabilionea Kwa Kutegemea kuuza nyimbo Tu.

Kwa nchi ya tanzania yenye high level of music piracy ni vigumu Sana msanii kuuza na kusimamia KAZI zake mwenyewe.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
We jamaa unaandika vitu kwa story za uswahilini, ningekua na time ningeku-quote one by one na nikakupa links ukaangalie facts.


Ila kiufupi ni hivi,
Kila app unayoona inafanya biashara lazima ina business model yake kwa nyuma pamoja na tech inayoisupport. business model au tech ikifeli basi biashara haiwezi kuzalisha revenue,

Soulja boy platform yake pamoja na nyingi za zamani zilikufa kwa sababu zilikua zinatumia old tech ya adobe flash kuplay hizo media, hio tech ikaanza kufa na ikakosa support kwa maker wake, sasa users watatumiaje kama platform yako ni ngumu kutumika? Hapo hata kama business model ni nzr basi unakuwa irrelevant kwenye market, na market siku zote ni 'MERCILESS' ikija issue ya 'IRRELEVANT PRODUCTS'.

Kuhusu halftime shows naona hujui chochote khs maandalizi ya hio show sababu hio show huwa iko kwa ajili ya kumpromote msanii, na nenda google ukaulize msanii gani ashawahi kulipwa kwa kuperform pale uje hapa unambie.

Huwa muandalizi wa mashindano anaweka bajeti fln lkn kama msanii anaeperform akiona haitoshi ndipo anaongezea pesa yake mfukoni sababu hio show ni maalum kumtangaza msanii anaeperform pale.

Bongo watu wengi wanapenda kucomment kwenye mambo bila kufanya research, ndo maana hata Mar Ruge aliwah kusema Fiesta haikupaswa kuwa inamlipa msanii, labda msanii ndo amlipe Fiesta. Sababu hizo shows marekani wasanii wanalipia ili kuperform.

Mfano wako wa UBER siwezi ongelea kwa sababu ni tofauti kabisa na kinachoongelewa hapa, ni business mbili tofauti kabisa, model zao kufanana ni ngumu sana
 
Jinga kweli wewe !


Watu mafuta ya petrol yakpanda bei Kwa 500 nchi nzima kelele unasema wanaweza kulipia subscription za YouTube...


Mchele na maharage yako Kwenye highest price watu wanalia ndio waweze kulipalia YouTube monthly, unachekesha Sana wewe

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Huna akili

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Unaongelea piracy lkn hujasoma comment zangu vzr chief.

Kuhusu piracy nimesema wakiamua kutengeneza platform itakayolinda kazi zao haishindikani, kuna technology kama NFT zinazotumia blockchains, na hilo nmesema kwenye moja ya comments zangu hapo juu. Anyway hio inakua too technical tunaweza tusielewane,

Lkn trust me, piracy ya US na ya BONGO ya bongo chamtoto, naongea hilo kutokana na experience. Ushajiuliza torrent wametengeneza wabongo au US? na ndio tech inayoliza hadi media production companies kubwa.

Piracy ya kibongo kuithibiti ni rahisi saaaaaaana kama kumsukuma mlevi. Kuna kitu kinaitwa DMCA, wasanii wa bongo hawaitumii na ndo maana wanalia lia, hio ni solution kwa piracy ya mtandaoni. Piracy ya vituo vya flash wasanii wanakua wajinga kutumika kisiasa, kwa nn wasikomalie serikali ipige stop hizo mambo? Kama waliweza stop matumizi ya mifuko ya plastik watashindwaje hilo.

Nmejibu hoja zako chief, nijibu kwa hoja au tuishie hapo
 
Mchele na maharage yako Kwenye highest price watu wanalia ndio waweze kulipalia YouTube monthly, unachekesha Sana wewe
Kama wewe huwezi kulipia kuna watu wanalipia.

Shida huna facts.... unaiga maneno ya watu tu badala ya kutafuta facts
 
Ila nawaza,yani Diamond huyu huyu nnajemjua Mimi awe hajawaza wazo la mtoa mada,lazima kuna kitu tusichokijua.
 

kutokana na umaskini wetu utube sio rafiki kwetu.

platform za bongo malipo huwekwa siri kwa sababu ni kidogo.
spotfy, i tunes na apple wanalipa vizuri na malipo yao yapo wazi.

wasanii washakuwa maarufu hawahitaji youtube kujulikana na kwenye soko la kimataifa utube sio njia bora zaidi. Ni lazima auze kazi zake apate pesa nyingi zimsaidie kujitangaza kwa namna bora zaidi.

hatuhitaji kuleta upinzani kwa utube bali platform ya kuuza kazi,uwekezaji wameshaufanya kwenye majina yao.
 
Sasa unataka kusema kitu ameshindwa Soulja Boy ndio waweze wabongo hawa wanaoishi nyumba za kupanga na magari ya kukodi kwa car dealers? Ukijumlisha utajiri wa wasanii 10 wa bongo unafika hata nusu ya Soulja Boy?

Watu mnaojua makompyuta mnachukulia vitu kirahisi mkishaona kitu kinatengenezeka mnadhani kitafanya kazi vilevile na kupenda kuigaiga. Kama ni hivyo Vevo si ingejitegemea tu kwanini iwe na contract na YouTube?

Na hilo yowe lote unalopiga umelitoa kwenye paragraph moja niliyoandika:
"YouTube ni platform ya kutafuta kujulikana zaidi wala sio kutengeneza hela uko, kujulikana kwenyewe kunaleta hela baadae. Nadhani ushajua kwanini Rihanna hakulipwa kwenye Super Bowl, wala hakuna msanii anayelipwa uko tena wengine kama Ed Sheeran na J Cole walitoa hela zao mfukoni kuongezea kuandaa show."

Nilimaanisha YouTube ni kama platform ya kukupa mashabiki na ukalipwa kidogo, nikatoa mfano wa Super Bowl kama platform ya kukupa mashabiki ndio maana hawalipi msanii. Na maelezo yangu yametosheleza kabisa ila kwa ujuaji wako na kudhani wewe ndio mwenye akili pekee ukarudia kilekile niichosema.
Na suala la Fiesta unalosema ndio hiyohiyo hoja yangu.

Dunia hii sijawahi ona msanii anapata utajiri kupitia YouTube au streaming platforms kama Deezer, Spotify na Apple Music.

Hawa wasanii wasio na uwezo wa kuendesha record labels ndio unataka waunde platforms zao? Marekani rappers kibao wana labels zao na contracts na giants kama Sony, Warner na Universal. Mmemtaja Jay Z na Roc A Fella.
Rick Ross ana Maybach Music Group ilikuwa na kina August Alsina, Meek Mill, French Montana, etc.
Lil Wayne ana Young Money imewatoa kina Drake, Nicki Minaj na wengine. Na rappers zaidi ya 20 wana labels hata Young Thug wa juzi tu hapa ana Young Stoner Life na wahuni wake. Sasa hawa wote wenye hela ndefu washindwe waje waimba you go blast mai medula ndio waweze?

Mnataka mfirisi watu nyie, msifanye hiki ni kitu rahisi. Inawezekana ila sio kwa hela walizonazo wasanii mpaka investors na akili kubwa wakae kuteseka miaka na miaka
 
Hao wasanii wenu huwa wanarudisha nini kwa jamii,au ndy mnawakamua kwa matamasha yenu kwa viingilio
Mnataka nyie tu ndiyo mpate

Ova

wasanii wetu hawawezi kurudisha kwa sababu wanachopata ni kidogo.
huyu diamond huwa anajaribu kwa kidogo hichohicho nadhani kama unafuatilia utakuwa unaelewa.
alikiba naye alijenga msikiti.
maana yake nini, kama wakitengeneza mazingira ya kupata zaidi nao watarudisha zaidi.
 
Sidhani kama YT inawahitaji kuliko inavyowahitaji.
Halafu wabongo wagumu nunua kazi ndio maana ile platform ya diamond ya kuuza nyimbo haikuchukua hata miezi sita ilikiwa ishapotea

youtube ina faida ndogo sana kwa msanii wa bongo.
shida ya ile platform ya mond ni kuuza kazi wakati bado inapatikana bure kwenye platform nyingine ambayo ni youtube.
 
Wazo ni zuri ila sasa utekelezaji wake ni ghali sana kulingana na tabia ya watumiaji wa bidhaa na huduma za wasanii wetu, uuzaji holela wa kazi za wasanii bado ni mwiba mkali yani mambo ni mengi mkuu.

ndio maana nikachukua kwa just a part of fans.
mfano out of 8m alikiba instagram fans alionao, akawa na loyal fans 2m wakanunua kazi yake kwa 200 anapata 400m hapo chap.
 
youtube ina faida ndogo sana kwa msanii wa bongo.
shida ya ile platform ya mond ni kuuza kazi wakati bado inapatikana bure kwenye platform nyingine ambayo ni youtube.
Mkuu, unajua kwa sasa watu wanasikiliza nyimbo baada ya kuzisikia ndipo wanaenda kuzifuatilia. Ukisoma comment nyingi za YT utakuta watu wanasema walianzA kuzisikia Tiktok ndo wakaja zitafuta YT.
Biashara imebadilika, ndio maana wameamua kuwa wanaachia nyimbo bure ziwe viral wapige show au wapate views.
Kwa sasa hii ndio business model inayolipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…