Wengi tuliamini Jeshi la Polisi linahusika Kuteka na kutesa watu hasa Wenye kukosoa serikali katika Mambo mbalimbali. Lakini Jana IGP CAMILIUS WAMBURA akiwa Bariadi ameta.ka Wazi kabisa Polisi wake hawahusiki. Na ametoa mifano ya Mtoto wa Mbeya aliyetekwa Kwa maelekezo ya mama yake ili apate hela toka Kwa mzazi mwenzie na watoto wawili wa Mwanza mkubwa akiwa na miaka 12 waliojiteka na kupanga chumba ili wapige hela Kwa mama yao mzazi lakini Kwa weledi wa hali ya juu kabisa Polisi wa Bwana Wambura wakategua mtego ule na kuwakamata.