Nawasikitikia sana wazazi wenye vipato vya kati mnaojitesa kuwasomesha watoto wenu (Gen Z) kwenye shule za mamilioni

Mzee kwan mtaala wa elimu umebadilika kias hicho? 90% ya ulioyasoma na ndio hayo wanasoma tena wao yamepungua viwango. Mtihani wa mathematics wa form 2 leo hii sis ndio zilikua test za form 1.
Acha uongo,mitaala ya ya sasa imeboreshwa hasa kwenye sayansi kwani Kuna mambo yamebadilika sana.
 
Halafu shule bora kwa mtazamo wangu sio zenye gharama kubwa au zilizofaulisha.Mimi huwa nampeleka shule mtoto zile shule za kati yaani zenye ufaulu wa division 1 ,2 ,3 ,4 na hata zero kwa uwiono.Ili awe na network ya kila Aina ya watu na shule ya namna hii ndio iliyofundisha sasa.
 
T

Tumia akili wewe fala mleta uzi amesema wazi kuwa familia za uwezo wa chini ndiyo ziwe makini kusomesha watoto kwenye shule za gharama kubwa ...foolish
Kipato cha chini anawezaje kusomesha shule ya gharama kubwa? Wewe ndie kichwani hazimo

Kinachoamua MTU asome shule ya gharama kubwa NI kipato

Unashaurije sasa MTU mwenye kipato kidogo asisomeshe shule ya gharama kubwa wakati kipato chake hakiruhusu

NI paradox ushauri wako umekaa kibwege

MTU akisonesha shule ya gharama kubwa ujue kipato chake zinaruhusu sababu kule hawasoneshi bure

Huo ushauri NI hewa hakuna mwenye kipato kidogo awezae somesha shule ya gharama kubwa
 
Wewe ni liongo sana smart phone gani inakosa password??
 
Wako watu wanaishi uswahilini tunawajua wanasomesha watoto wao kwenye hizo shule kama uamini nenda kwenye hizo shule utakuta tatizo la ulipaji ada kwa baadhi ya wanafunzi ..wazazi wao wanaungaunga kulipa
 
Tanzania hii hakuna shule yenye elimu bora. Labda kwa zile shule chache ambazo hazitumii mitaala ya Tanzania. Tofauti ya English Medium na na hizi za kawaida (Kayumba) ni matumizi ya lugha tu ila mitaala au kiwango cha ubora wa elimu kiko sawa.
Mzazi mwenyewe achague sehemu sahihi ya watoto wake kusoma.
Ushauri wangu kwa wazazi wenzangu, tusipoteze pesa nyingi kwenye shule zinazojinasibu ni bora maane kadiri mtoto anavyosogea mbele watakutana kwenye Form 5, Diploma na Bachelor. Katika hayo madaraja ndio utagundua hakuna tofauti kati ya Kayumba na hizo zingine.
Kwa hiyo, wazazi tutumie busara katika kuwasomesha watoto wetu. Tujikite katika kuwekeza zaidi ili hao watoto wakipata elimu zao wawe wasimamizi wa miradi tuliyowekeza. Sasa wewe poteza mahela kibao mwanao akimaliza elimu yake aanze kuhangaika kutembeza bahasha. Badala ya kutumia pesa nyingi kusomesha, wekeza ili huyo mtoto akihitimu anaingia kwenye ajira ambayo umeshaitengeneza.
 
Ni kweli sipotezi hela na toa ml 1 tu kwa ada ya mwaka kwa watoto sitaki apelekwe na basi ajue atarudije au kitamwambia mtu akamchukue au aingie dalala kuna njia ambayo nitamtafutia arudi home ila 2. 5 to 20 ml huo ni ukichaa na biashara za kufanya
 
Wewe ni liongo sana smart phone gani inakosa password??
Kila mwenye smart phone anakuwaga na password?

Mtoto wa miaka 14 anaweza kuweka password kwenye simu yake?

Unaishi kwa kukariri eeh? Unauliza kwa nini sijavaa mkanda wakati suruali hainibani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…