Nawatakia kila la kheri watani kwenye silent war in Dar

Nawatakia kila la kheri watani kwenye silent war in Dar

Joined
Aug 15, 2013
Posts
55
Reaction score
23
Miongoni mwa mechi muhimu kwa kundi A kwa mtani wetu ni hii ya leo dhidi ya Al-merekh.

Maana baada ya mechi hii ambayo kiuhalisia ndio ya kuvunia point na kutangaza rasmi kufuzu Hatua ya robo fainali.

Ni muhimu kufanya vizuri kwenye mechi hii kwa maana baada ya mechi hii zinazofuata ni mechi ngumu na zitakazokuwa na mvutano mkubwa wa kugawana point.

Mbaya zaidi fitina zimeanza kwa kuwazuia mashabiki wa mtani kuingia ndani ya Mkapa stadium.

Tukutane SAA 10:00 kwa Mkapa
WENYE AZAM ZETU
IMG-20210301-WA0029.jpg
 
Simba wakishinda leo watahitaji point moja tu dhidi ya As Vita ndio ufuzu endapo mechi ya As Vita dhidi ya Al Ahly mmoja wapo atashinda leo
Haswaa,ila Vita Vs Al Ahly waki droo itakua poa sana,lakini Simba leo ashinde,akipigwa au kudroo haaa basi ndo itakua imeisha imeisha iyo.
 
Simba wakishinda leo watahitaji point moja tu dhidi ya As Vita ndio ufuzu endapo mechi ya As Vita dhidi ya Al Ahly mmoja wapo atashinda leo
Simba wakishinda Leo watakua wamefuvu moja kwa moja

Angalia wanaomfata nyuma afu tabiri matokeo yao endapo mmoja akishida maana yake hawezi zifikia point za Simba na endapo wakidroo ndo watakua wameongeza zaidi Vita za wao kwa wao
 
Ipo hivi:. Simba wakishinda leo watakuwa na alama 10 na mechi mbili mkononi. Ya kwanza ni vs As Vita kwa Mkapa na ya pili vs Al Ahly itakayochezwa Misri.
Endapo mechi ya leo As Vita vs Al Ahly, Akishinda As Vita itampa As Vita nafasi ya pili kwa kuwa na point 7
Mechi inayofuata Simba anatakiwa ashinde au atoe sare ili awe na point 11 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote. Kwasababu wakati Simba ikicheza dhidi ya As Vita, Al Ahly wao watakuwa wakicheza na Al Merreikh ambapo wakishinda Al Ahly watafikisha point 7 nao.
Hivyo Kama mechi ya Simba vs Vita, Simba wakiikosa alama moja au zote tatu maanake sasa
Simba watakuwa na point 10
As Vita point 10
Al Ahly point 7

Simba itaenda kucheza mechi ya mwisho misri huku Al Ahly wakihitaji ushindi ili kufikisha alama 10 huku Simba ikiwa inahitaji alama moja kufikisha point 11
Na pia As Vita wakiwa nyumbani anamaliza dhidi ya Al Merreikh huku wakiwa wana point 10 kama ilivyo kwa Simba.
 
Oya huu uzi ubadilishwe Heading ili utumike kujuzana updates.
Kila la kheri Mnyama
 
Back
Top Bottom