Nawatakia waadventista wasabato na waumini wa dini ya kiyahudi siku ya mapumziko (sabato), Tuendelee kutii amri kumi bila ubaguzi

Sawa. Sasa mwinjilisti Musa alipotoka kule mlimani na zile Amri 10 mbona hakuwapa makabila mengine yaliyokuwepo mengi tu kuwaambia washike sabato. Aliwaambia Waisrael tu.
Sabato ni kwa wayahudi tu

Kama na wewe unataks kushika sabato basi ka nayo wewe, kuwahubiria wenzako unapoteza Muda.

Ndio maana Mtume Paulo alikuwa anahubiri injili na Timoteo ambae ana govi hajatahiriwa kama maagizo ya package ya maagano ikiwemo Amri 10.
Alimtahiri kuwafurahisha tu wayahudi.
Kidogp kidogo utaelewa mkuu.
Sabato ni kwajili ya watu wote wanaoamini Mwnyezi Mungu aliumba dunia kwa siku sita, ya saba alipumzika na yeye akaturuhusu nasi tupumzike siku ya saba.

Kwa enzi hizo Waumini walikuwa waisrael, sehemu nyingi ikiwemo Afrika tulikuwa tuna imani tofauti kabisa.

Hata ukristo umeingia Tanzania baada ya miaka 1900
 
Basi tunakubaliana Sheria imebadilika kutia Ndani maagizo ya sabato Ile waisraeli walishika hii ni tofauti maana haitii maagizo yote ya Musa😊

Hilo Lina maana Sana na ndio Jambo kuu kapitie tena kitabu cha waebrania
Sabato ya sasa ni ile aliyoikuta hata Yesu, Hakukuwa na mtu alieuliwa siku ya sabato.

Unachozungumzia wewe ni adhabu za hapo zamani sana zilizokuwa kali mno, sio kwa kuto abudu siku ya sabato tu bali amri nyingi ukivunja adhabu zilikuwa kali.
 
Sabato ni kwajili ya watu wote wanaoamini Mwnyezi Mungu aliumba dunia kwa siku sita, ya saba alipumzika.

Kwa enzi hizo Waumini walikuwa waisrael, sehemu nyingi ikiwemo Afrika tulikuwa tuna imani tofauti kabisa.

Hata Yukristo umeingia Tanzania baada ya miaka 1900
Sasa Timoteo kutotahiriwa si alikuwa najis na kwa hali hiyo asingekuwa anafaa kwa sabato na alikuwa bega kwa bega na Mtume Paulo. Wewe unazani Mt. Paulo alijisahau.
 
Sabato ama ka neno lake asili la kiyahudi shabbāth ni neno lenye kumaanisha mapumziko

Mwenyezi Mungu kaweka amri ya kuitakasa siku ya Sabato ndani ya zile amri 10, ni jambo kubwa sana kwetu, Ni kibali kitakatifu kinachotupa ruhusa ya kupumzika siku moja kila wiki ya siku 7. Utaratibu wa kuiabudu siku hii ulianza tangu enzi za Musa alieaminiwa na Mungu kwenye mambo mengi ikiwemo kumkabidhi amri zake kumi, Yesu aliisifu sabato na bado mpaka leo inaabudiwa Israel na madhebu machache ya kikristo kama waadventista wasabato.

Ni ishara ya Upendo Mungu katupa siku hii tupuzike, Nasi pia turuhusu wafanyakazi wetu tuliowaajiri wapumzike, mifugo yetu tunayotumia kwenye shughuli zetu nayo ipumzike.

Katika mapumziko haya tusisahau kurudisha fadhila hii kwa kumuabudu alietupa siku hii, tukutane sehemu za kumuabudu tumuimbie nyimbo za kumsifu, kusali, n.k. kisha kurudi makwetu kuendelea na mapumziko

Yesu alizitii amri 10 na aliisifu siku ya sabato na kutusihi zaidi tuwe na upendo, hivyo hatuna budi tufuate njia zake

Shetani toka pepo ingia, na wote tuseme tawire 🙏
 
Sasa Timoteo kutotahiriwa si alikuwa najis na kwa hali hiyo asingekuwa anafaa kwa sabato na alikuwa bega kwa bega na Mtume Paulo. Wewe unazani Mt. Paulo alijisahau.
Ukitaka sabato isikuchanganye sana wewe tilia mkazo maana ya nenio "Kupumzika", Ni siku takatifu kwetu kupumzika, twarudisha fadhila kwa kuabudu
 
Sabato ya sasa ni ile aliyoikuta hata Yesu, Hakukuwa na mtu alieuliwa siku ya sabato.

Unachozungumzia wewe ni adhabu za hapo zamani sana zilizokuwa kali mno, sio kwa kuto abudu siku ya sabato tu bali amri nyingi ukivunja adhabu zilikuwa kali.
Yoh 5:18 Basi Wayahudi wakazidi kutafuta njia ya kumuua, kwa sababu hakuwa tu akivunja Sabato bali pia alikuwa akimwita Mungu Baba yake, akijifanya kuwa sawa na Mungu.

Ilikuwepo Sana Tu! Na watu waliuwawa Kama Stefano alipigwa mawe
 
Ukitaka sabato isikuchanganye sana wewe tilia mkazo maana ya nenio "Kupumzika", Ni siku takatifu kwetu kupumzika, twarudisha fadhila kwa kuabudu
Unatoa maelezo ambayo sio sawa unakazia kupumzika kama wasabato wote.
Baada ya Muumba kupumzika siku ya saba na kuitakasa hiyo siku hakusema sasa sababu mimi nimepumzika na wanadamu wote wapumzike. Hakuna mahali katoa tamko hilo kabla ya kule mlimani kwa Musa.
Ina maana Adam na Hawa hawakushika hiyo sabato, wala Ibrahim, Isaka, Yakobo na watoto wake, Nuhu, Luti .

Ilitoka Jangwani kupewa wayahudi tu.

Baada ya Yesu kuondoka wayahudi waliomfuata Yesu waliendelea kushika sabato, sasa wale "mataifa" au watu wengine walioamua kumfuata Yesu ambao hawakuwa wayahudi hawakuaambiwa watahiri siku ya nane watoto wao au wenyewe au washike sabato, walifuata mafundisho ya Yesu kama yalivyo.
Kifupi ndio maana ulitokea mvutano Paulo na Petro. Paulo akimtuhumu Petro kutaka kuwafanya waumini wasio wayahudi waishi na kufuata desturi za kiyahudi (torati) kama wewe unavyofanya,lakini wewe nadhani hujui, umekariri ulivyofundishwa.
 
Sabato ama ka neno lake asili la kiyahudi shabbāth ni neno lenye kumaanisha mapumziko

Mwenyezi Mungu kaweka amri ya kuitakasa siku ya Sabato ndani ya zile amri 10, ni jambo kubwa sana kwetu, Ni kibali kitakatifu kinachotupa ruhusa ya kupumzika siku moja kila wiki ya siku 7. Utaratibu wa kuiabudu siku hii ulianza tangu enzi za Musa alieaminiwa na Mungu kwenye mambo mengi ikiwemo kumkabidhi amri zake kumi, Yesu aliisifu sabato na bado mpaka leo inaabudiwa Israel na madhebu machache ya kikristo kama waadventista wasabato.

Ni ishara ya Upendo Mungu katupa siku hii tupuzike, Nasi pia turuhusu wafanyakazi wetu tuliowaajiri wapumzike, mifugo yetu tunayotumia kwenye shughuli zetu nayo ipumzike.

Katika mapumziko haya tusisahau kurudisha fadhila hii kwa kumuabudu alietupa siku hii, tukutane sehemu za kumuabudu tumuimbie nyimbo za kumsifu, kusali, n.k. kisha kurudi makwetu kuendelea na mapumziko

Yesu alizitii amri 10 na aliisifu siku ya sabato na kutusihi zaidi tuwe na upendo, hivyo hatuna budi tufuate njia zake
b1aa63434161f222323011896ae463bf.jpg
 
Back
Top Bottom