Nawatakia Wakenya wote uchaguzi mwema, wenye amani na wa haki

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325
Wakenya watapiga kura katika uchaguzi mkuu hapo 4 Machi,2013 kwa mara ya kwanza tangu kupitishwa kwa katiba mpya mwaka 2010.

Uchaguzi utajumuisha wagombea 1,882 kwa nafasi za kuchaguliwa, ambazo kama sijakosea ni nafasi moja ya urais, wabunge 290, maseneta 47, magavana wa majimbo 47, wawakilishi wanawake wa majimbo 47 na kata za uraia 1,450.

Nikiwa kama Mtanzania, ningependa kuchukua nafasi hii kuwatakia Wakenya wote kila la heri kwenye uchaguzi huu. Hii ni nafasi ya kila Mkenya kutumia haki yake ya kupiga kura. Ni matumani yangu kuwa Wakenya watafanya uchaguzi mwema, wa haki na amani.

All the best and save yourself. Vote.

Last edited by a moderator:
These people should vote wisely and accept the results we never want to see that their last election scene again!if it is true what we are hearing that they have already bought swords and pangas .......they should bury them!
 
Clip number one must seen ... "Intertaiment yote iko kwa Bibi Peke yake.." Hah aha!!
 
NTV LIVE | KenyaMOJA.com
tunajifunza nini kwa hawa wenzetu wa kenya? Uhuru Park na Nyayo stadium
TV zao zinaonyesha kwa pamoja matukio tofauti live katika kipindi hiki cha mwisho wa kampeni
wachambuzi wanachambua kwa usawa sera za kila chama
 
Hamna cha kujifunza hapo, wewe vuka boda tu hamia huko kama vipi! Kila nchi utamaduni wake na na namna yake ya kufanya mambo yake, wao wanafanya hivyo, sisi hatufanyi hivyo na maisha yanaendelea na mwisho wa siku Mtanzania wa kawaida ana maisha ya raha kuliko Mkenya wa kawaida ambaye hajui kuanzia J3 kama mtoto wake atarudi salama kutoka shule au vipi?

Mimi nasubiri tu kiwake huko waanze kuchapana, kwa miaka 5 mfululizo, halafu tuwapite Kiuchumi, hahahah!

Kila la Heri Jumatatu jirani!

jaribu kuwasikiliza wnavochambua siasa ndio uanze kukoment hapa
wachambuzi wao wana weledi mkubwa kisiasa
wanaelewa ni nini wanachopaswa kuwaeleza watazamaji bila ubaguzi
sio kama wachambuzi wa TVzetu za bongo wanaoshabikia zaidi uchama kama TV ya Taifa TBC na zingine
ya kujifunza yapo mengi sana ukiwasikiliza kwa makini
kwa wakati mmoja utawana wanazungumzia kampeni zote na kuwaonyesha live pamoja.
ndivo walivokuwa wanafanya CNN, ABC wakati wa kampeni uchaguzi marekani
Hamna cha kujifunza hapo, wewe vuka boda tu hamia huko kama vipi! Kila nchi utamaduni wake na na namna yake ya kufanya mambo yake, wao wanafanya hivyo, sisi hatufanyi hivyo na maisha yanaendelea na mwisho wa siku Mtanzania wa kawaida ana maisha ya raha kuliko Mkenya wa kawaida ambaye hajui kuanzia J3 kama mtoto wake atarudi salama kutoka shule au vipi?

jaribu kuwasikiliza wnavochambua siasa ndio uanze kukoment hapa
wachambuzi wao wana weledi mkubwa kisiasa
wanaelewa ni nini wanachopaswa kuwaeleza watazamaji bila ubaguzi
sio kama wachambuzi wa TVzetu za bongo wanaoshabikia zaidi uchama kama TV ya Taifa TBC na zingine
ya kujifunza yapo mengi sana ukiwasikiliza kwa makini
kwa wakati mmoja utawana wanazungumzia kampeni zote na kuwaonyesha live pamoja.
ndivo walivokuwa wanafanya CNN, ABC wakati wa kampeni uchaguzi marekani

Acha kusifu vitu usivyovielewa, Wakenya wana kesi ya kujibu huko Mahakama ya kimataifa ya Hague, na hao hao wahandishi wa Habari wa Kenya unaowasifu ndio walio sababisha watu zaidi ya 1000 kuchinjwa live kama wanyama, sasa hata kama wahandishi wetu hawako kama wa CNN lkn hawachochei watu kuchinjana na wala hawana kesi za mauaji!

Ndugu wanaJF!
Wengi tunaelewa kwamba jirani zetu na marafiki zetu wa Jamhuri ya Kenya wanelekea kufanya uchaguzi wao kesho tarehe 3.3.2013.
Tunajua jinsi chaguzi nyingi hasa za Afrika hufuatiwa na vurugu kubwa ambazo husababisa upotevu wa mali na maisha.
Nawaomba wanaJF wote, tuungane kwa pamoja kuwaombea hawa ndugu zetu wawe na uchaguzi mwema hapo kesho.
Amani ya Kenya ni Amani ya Tanzania, Rwanda, Uganda, DRC na Afrika kwa ujumla.

Kila la kheri kwa wagombeaji wote katika uchaguzi wa Kenya.
Kila la kheri wapiga kura wote katika uchaguzi wa Kenya.
Kila la kheri kwa Wakenya Wote.

Harambeeeee!
Nyayooo!
 
K24 inampendelea zaidi kumwonesha Uhuru kuliko Raila.
 
NTV LIVE | KenyaMOJA.com
tunajifunza nini kwa hawa wenzetu wa kenya? Uhuru Park na Nyayo stadium
TV zao zinaonyesha kwa pamoja matukio tofauti live katika kipindi hiki cha mwisho wa kampeni
wachambuzi wanachambua kwa usawa sera za kila chama
ni somo kwa vyombo vyetu kujifunza kwa wenzao wa kenya,hapa nchini vyombo vingi vimejaa unafki mwingi kwa serikali ya ccm,ukiangalia kipindi cha dk45,cha itv kila siku ni watu wa ccm mawaziri wale wale mpaka tunajiuliza ikikipindi ni cha watu wa ccm,au wamelipia wao,kama awajalipia je akuna watu wengine katika jamii wanaofanya mambo mazuri wawa alike waje kwenye kipindi cha dk45 cha itv,tuliona kwenye kampeni za 2010,tv stesheni hazikuwa fear kwa vyama vya upinzani,tofauti na ccm,tunamshukuru aliekua mkurugenzi mtendaji wa tbc bwn,tido mwando kwa kutuletea mjadala live kutoka majimbonii,,,nandio ilikua kaburi lake kuondolewa,tbc,nadhani hathari za kuondolewa tido tbc,zinaonekana tbc sasa imekua [tbccm]mikutano ya ccm wanakesha tena live,sasa kimekua ni chombo cha makala za ccm na kupiga propaganda chafu kwa upinzani hasa chadema hata habari za chadema ni mwiko kusomwa au kuonyeshwa kwenye habari zao,mwisho vyombo vyote vya habari vijue wananchi wanauwezo wa kukiweka chama watakacho amua kukiweka,sasa basi vile vyombo ambavyo vilikua adui wa chama ichoambacho kitawekwa madarakani katika uchaguzi ujao 2015 watafute shimo la kuingilia,itakua bonge la sinema, maana wale ambao waliwafanya vibaraka watakua wameondolewa[tbc][itv][star tv]chanel 10]na nyingine akili vichwani mwenu dalili zipo wazi kwamba ccm bye bye,
 
Hamna cha kujifunza hapo, wewe vuka boda tu hamia huko kama vipi! Kila nchi utamaduni wake na na namna yake ya kufanya mambo yake, wao wanafanya hivyo, sisi hatufanyi hivyo na maisha yanaendelea na mwisho wa siku Mtanzania wa kawaida ana maisha ya raha kuliko Mkenya wa kawaida ambaye hajui kuanzia J3 kama mtoto wake atarudi salama kutoka shule au vipi?

Gamba wewe
 
Ndugu wanaJF!
Wengi tunaelewa kwamba jirani zetu na marafiki zetu wa Jamhuri ya Kenya wanelekea kufanya uchaguzi wao kesho tarehe 3.3.2013.
Tunajua jinsi chaguzi nyingi hasa za Afrika hufuatiwa na vurugu kubwa ambazo husababisa upotevu wa mali na maisha.
Nawaomba wanaJF wote, tuungane kwa pamoja kuwaombea hawa ndugu zetu wawe na uchaguzi mwema hapo kesho.
Amani ya Kenya ni Amani ya Tanzania, Rwanda, Uganda, DRC na Afrika kwa ujumla.

Kila la kheri kwa wagombeaji wote katika uchaguzi wa Kenya.
Kila la kheri wapiga kura wote katika uchaguzi wa Kenya.
Kila la kheri kwa Wakenya Wote.

Harambeeeee!
Nyayooo!

Tunawatakia wewe na nani? Si usemee nafsi yako?
 
Back
Top Bottom