Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,503
Nadhani issue isiwe kukataa kujifunza hata vitu vizuri kutoka kwa wengine.
Kama mpango huo wa kuwapima wagombea wetu vizuri na kuamua uwezo wao na dira zao, ni kitu kizuri sana cha kujifunza, na sioni aibu kusema kuwa ni vema KUIGA.
A wise man changes his mind sometimes, a fool never.
Kwa hili hata mimi sikatai hata kidogo. Achilia mbali nchi, binadamu kila kukicha tunajifunza na ndiyo njia ya kupambana na changamoto za kimaisha. Lakini vile vile, kama jamii, tuna miiko na taratibu na sheria zetu tulizojiwekea kama taifa.
Kitu ambacho kwangu ninakiona ni absurb, ni hii kasumba ya kuona kama sisi hakuna kitu ambacho tumesimama na wengine wanataka kuwa kama sisi. Ukiangalia comment za Watanzania wengi hapa, utagundua wako negative kwa kila kitu nchini kitu ambazo kiuhalisia siyo kweli hata kidogo.
ni kweli, kuna kitu tunaweza tukajifunza kutoka Kenya lakini siyo vyote na Wakenya nayo wana kitu wanaweza kujifunza kutoka kwetu.
Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini ulitanguliwa na mdahalo wa wagombea Urais, kutokufanyika mdahalo kwenye last election isiwe ndiyo nyongwa. Hili ni jambo la utaratibu wa kisiasa kati ya chama na chama.
