Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Kwa heshima na taadhima, nichukue nafasi hii ya kipekee kuushukuru uongozi mzima wa jamii forums, wafanyakazi wake wote, na pia wana JamiiForums wenzangu kwa kuwa pamoja kwa mwaka wote huu wa 2024.
Natambua fika tumepitia mengi ndani ya mwaka wote huu. Wako ndugu na jamaa zetu wengi kwa namna moja au nyingine wameshindwa kuifikia hii siku ya leo. Lakini kwa upande wetu tunashukuru kufika salama pamoja na changamoto zetu mbalimbali za kiuchumi, kimaisha, kijamii, nk. zinazotukabili.
Lengo la huu uzi ndugu zangu, ni kutaka tu kuwatakia Wana jamii forums wote Heri ya Mwaka Mpya wa 2025! Natambua fika kuna baadhi yenu niliwakosea kwa namna moja au nyingine! Lakini pia kuna wachache wenu mlinikosea kwa kunikejeli, kunitukana, kuutweza utu wangu, nk. Binafsi napenda kusema nimewasamehe.
Hivyo na nyinyi nawashauri mfanye hivyo hivyo, ili maisha nayo yaendelee.
Mwisho kabisa napenda kuupongeza uongozi wa jamii forums kwa kufanikiwa kuufanya huu mtandao kuwa sauti ya wananchi walio wengi. Na uwepo wa viongozi waandamizi wa serikali, uwepo wa taasisi mbalimbali za serikali, nk. humu jukwaani, ni ushahidi tosha jamii forums ni chombo makini cha kupashana habari.
NB: Rai yangu ni kwa sisi wajumbe tuliomo humu jukwaani! Tujitahidi ndugu zangu kutoa maoni yetu kwa staha. Matusi, kejeli, nk. Ndiyo baadhi ya vitu vinavyoweza kutuweka matatani.
Lakini pia ninaomba ndugu zangu muwe mnanichukulia wakati fulani kutokana na ukweli kwamba mimi ni mtu ambaye huwa ninapenda kuchekesha kadamnasi, kuuliza maswali ya hapa na pale ya kufikirisha, nk. Therefore, don't take each and everything in a serious way, ok?
All in all, tukutane 👉 2025 panapo majaliwa. InshaAllah!
Wenu Tate Mkuu... Kutoka Lushoto Tanga.✍️
🙏