Nawatakieni Simba kila lenye heri kwenye siku yenu (Simba Day). Kiroho safi, Pokeeni zawadi kutoka Yanga

Nawatakieni Simba kila lenye heri kwenye siku yenu (Simba Day). Kiroho safi, Pokeeni zawadi kutoka Yanga

PakiJinja

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
11,689
Reaction score
25,848
Michezo ni furaha, michezo ni umoja. Naomba nichukue forsa hii kuwatakia Mashabiki, Wapenzi, wachezaji, viongozi, wanachama wa Simba kila lenye heri katika kuazimisha siku yao.

Mafanikio mtakayoyapata ni mafanikio katika familia ya soka, bila shaka kuna ambayo mlijifunza kutoka Yanga, mkajirekebisha kuelekea kwenye siku yenu ili ku improve, pia Yanga nao bila shaka kuna vitu watajifunza kutoka kwenu.

Kuigana na kufanya vizuri zaidi ndiyo ujanja na utimamu. Kuigana si dhambi ndiyo maana mnachukuliana wachezaji. Isingekuwa ushindani na kuigana, leo hii soka la Tanzania lisingefika hapa.

Katika kuwatakieni mafanikio mema ile kiroho safi, kwa niaba ya Wana Yanga wa Jamii Forums naomba mpokee Video hii ikatawale status zenu huko Whatsapp na kwingineko Mitandaoni.

Yanga na Simba ni Watani wa Jadi, siyo Maadui wa Jadi.

 
Asante kwa Niaba mkuu...

Huu NDIO mpira.
Hawa ndio Wadau tunao wapenda.

HII ndio maana HALISI ya UZALENDO.

FAIR PRAY.
 
Nakuunga mkono
Natumai mtani ataifurahia siku yenu
Kila la heri mtani
 
Back
Top Bottom