Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Hivi hata kama ni kweli mnachokiamini mtoa mada na asilimia kubwa ya wachangiaji waliopita, hamjui kuwa kili ni kipindi kinachoangaliwa na watu wa aina mbalimbali hususani masikini maana matajiri waliikwisha kuneemeka hawanaga muda wa kuangalia Tv!
Je,kama kipindi kilibuniwa ili kulitia hamasa kundi kubwa la wanawake waliokata tamaa ya kupambana na maisha kutokana na ukosefu wa mitaji? Huoni kama hizo shuhuda hata kama ni za uongo zinasaidia sana kuwatia moyo wanawake hivyo kuwahamasisha waendelee kupambana mpaka kieleweke kuliko kusubiri msaada wa mwanaume?
Jamani naomba tufikiri kwa mapana,tusijikite tu katika kuzihukumu hizo shuhuda bali tuangalie pia mchango wake katika kumuinua mwanamke kiuchumi
 
Utasikia nilianza kuuza karanga kwa mtaji wa 5,000/= tu Leo hii namiliki viwanda 10 kiukweli nashukuru sana Juice Kiriya
 
Kila anayehojiwa na Mtangazaji ' Critical ' na ninayempenda na kumkubali kabisa Siza wa Cloudstv 360 on Saturday wakiwa ' mubashara ' kabisa kutokea Mlimani City kuwa aelezee Historia ya Mafanikio yake hadi leo wamefanikiwa Kimaisha unaona tu wanazunguka zunguka huku mengi tukifichwa.

Nikilitumia sana ' jicho ' langu Kali la ' Kisaikolojia ' na kwa jinsi ninavyowakodolea hawa Wanawake wakiwa ' mubashara ' wanatiririka na wanaserereka naona Shuhuda zao za Kimafanikio hayo waliyonayo zimejaa ' Unafiki ' mtupu hasa kwa wawili mmoja wapo akiwa anapatikana sana Millenium Tower Kijitonyama na mwingine akiwa mara kwa mara humkosi katika Vipindi vyake Channel Ten ambao ' Channels ' zao za hayo mafanikio yao zina mkono wa ' Kimahaba ' wa waliokuwa na Mamlaka yao / wenye Nyadhifa zao hapa Tanzania.

Wito tu Kwenu ambao huwa mnapenda ' Kutudanganya ' kuhusu mlivyopata hayo mafanikio yenu itapendeza sana na hata kutushawishi zaidi kama siyo kutufundisha endapo mtakuwa mnatupa zile Shuhuda zenu halisi hata kama zinatisha au kutia aibu kuliko kudhani kuwa huu uwongo wenu hatutaugundua haraka.

Ngoja niendelee kuwaangalia na nizidi Kudanganyika. Kazi ipo hakyanani!

Nawasilisha.

Script story
 
Yule Malkia wa nguvu sijui shamim alikuwa anawadanganya wenzake kuwakopesha fedha kimtindo wa vikoba .
Naye alikuwa na blahblah zake kibao.
Kumbe nyuma ya pazia ni biashara ya ngada ya mume wake.
Wanawake wote wanaojitangaza malkia wa nguvu ni wangu waongo
 
Back
Top Bottom