Nawatazama hawa Wanawake waliofanikiwa kimaisha Clouds Tv, ila Shuhuda zao za Mafanikio hazinishawishi

Hivi hata kama ni kweli mnachokiamini mtoa mada na asilimia kubwa ya wachangiaji waliopita, hamjui kuwa kili ni kipindi kinachoangaliwa na watu wa aina mbalimbali hususani masikini maana matajiri waliikwisha kuneemeka hawanaga muda wa kuangalia Tv!
Je,kama kipindi kilibuniwa ili kulitia hamasa kundi kubwa la wanawake waliokata tamaa ya kupambana na maisha kutokana na ukosefu wa mitaji? Huoni kama hizo shuhuda hata kama ni za uongo zinasaidia sana kuwatia moyo wanawake hivyo kuwahamasisha waendelee kupambana mpaka kieleweke kuliko kusubiri msaada wa mwanaume?
Jamani naomba tufikiri kwa mapana,tusijikite tu katika kuzihukumu hizo shuhuda bali tuangalie pia mchango wake katika kumuinua mwanamke kiuchumi
 
Utasikia nilianza kuuza karanga kwa mtaji wa 5,000/= tu Leo hii namiliki viwanda 10 kiukweli nashukuru sana Juice Kiriya
 

Script story
 
Yule Malkia wa nguvu sijui shamim alikuwa anawadanganya wenzake kuwakopesha fedha kimtindo wa vikoba .
Naye alikuwa na blahblah zake kibao.
Kumbe nyuma ya pazia ni biashara ya ngada ya mume wake.
Wanawake wote wanaojitangaza malkia wa nguvu ni wangu waongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…