Nawauliza watumishi wa Yesu Kristo: Mungu Mkuu kupita miungu yote, aliye hai peke yake, kwa nini wanaoneana Wivu katika kazi walizopewa!?

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
habari ya wakati huu jamii forum
leo nawazungumzia hawa watumishi na ninaposema watumishi sio tu wahubiri wa neno la Mungu na na utendaji wa huduma zao, bali na waimbaji wa nyimbo za injili ambao wao wanahubiri kupitia nyimbo, ikiwa ni moja ya zile huduma tano alizotoa Yesu Kristo ya uinjilisti.

kuna wengine wanaimba nyimbo za kuabudu, wengine kusifu na kutukuza, wengine tenzi za rohoni. Lakini wote huduma yao ni moja ya uinjilisti. sasa itashangaza mmoja wa kuabudu anamuonea wivu wa kusifu na kutukuza, na wa kusifu ana wivu na wa tenzi za rohoni. Wanasahau kabisa huduma yao ni moja na wote kazi yao ni kurudisha mioyo ya watu kwa Mungu.

ni bora hata waimbaji wa nyimbo za injili, lakini hawa wafundishaji wa neno la Yesu Kristo, wivu umezidi kwa Huduma walizopewa na Roho mtakatifu.
ni kushambuliana tu wakitumia madhabahu walizopewa kwa ajili ya huduma.
Yesu Kristo aliacha huduma TANO kwa kanisa na huduma hizo ni:
1. Utume: mtu mwenye hii huduma huwa hakai sehemu moja ni kuzunguka huku na kule, kuufikisha ujumbe aliopewa na kazi aliyopewa kuifanya hata kama kuna sehemu anapatikana.
2. Nabii: mtu mwenye hii huduma ni Mtu wa Maono, Ndoto na Mafunuo.
watu hawa wamepewa kuona vitu vinavyokuja mbeleni kabla havijatokea na kujua vilivyopita hata kama hakuwa amezaliwa, na kukusaidia namna ya kuepuka ili usiingie pabaya.
3. wachungaji: watu hawa huwa wanapatikana sehemu moja tu. na ukiwa na shida nao ni rahisi kuwapata. wao kazi yao ni kuchunga kundi ambalo tayari analo.
4. wainjilisti: watu hawa ni watu wa maonyo, acha uovu unaofanya la sivyo ni 🔥 moto unaenda kukuchoma kama ambavyo unaenda kumteketeza anaewachochea, ambaye ni satani.
5. Ualimu: watu hawa ni wafundishaji wa NENO la Mungu. kwa undani wake na lengo ni watu kulijua neno la Mungu kiundani na kuirudisha mioyo yao kwa Mungu.

sasa kila mtu anaweza kupewa huduma yake na namna atakavyoitenda, lakini kuna wengine wanapewa zote kulingana na huyo mtu jinsi alivyo.au kutokana na neema aliyo nayo mbele za Mungu, kutokana na Roho mtakatifu apendavyo.
na kila mmoja ni ili kuwajenga watu kwa faida ya Mungu.
sasa nauliza Wivu wa nini, kwa nini usimwambie aliyekupa huduma, akakupa ubunifu zaidi ili huduma uliyopewa izidi kuwa kubwa na kujulikana.
watumishi walio wengi sasa hivi hawamuulizi Mungu, ndio maana huduma zao hazikui na wala hazijulikani. wamebaki kuwashambulia wenzao wachache ambao wanafunga, wanaomba na kukesha milimani kila wakati ili kuisikia sauti ya Mungu kuhusu huduma alizowapa na namna ya kuzitenda.
watumishi wa Mungu badilikeni, kumsema vibaya mtumishi mwenzio hakuifanyi huduma yako uliyopewa kukua.
 
Attachments

  • Screenshot_20241229-115950.png
    Screenshot_20241229-115950.png
    68.2 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241229-120111.png
    Screenshot_20241229-120111.png
    68.9 KB · Views: 2
  • Screenshot_20241229-120704.png
    Screenshot_20241229-120704.png
    71.7 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241229-121428.png
    Screenshot_20241229-121428.png
    84.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241229-121951.png
    Screenshot_20241229-121951.png
    96.2 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241229-122042.png
    Screenshot_20241229-122042.png
    82.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241229-122259.png
    Screenshot_20241229-122259.png
    80.2 KB · Views: 2
Wanaoneana wivu kwasababu wanajujua ni matapeli so utapeli wa mwenzako ukiwakolea watapeliwa maana yake pesa pia zinakuja nyingi!.
 
Mtume na Nabii wa Mungu aposto Mwamposa among other TAPELIZZ in town😂😂😂
 
habari ya wakati huu jamii forum
leo nawazungumzia hawa watumishi na ninaposema watumishi sio tu wahubiri wa neno la Mungu na na utendaji wa huduma zao, bali na waimbaji wa nyimbo za injili ambao wao wanahubiri kupitia nyimbo, ikiwa ni moja ya zile huduma tano alizotoa Yesu Kristo ya uinjilisti.

kuna wengine wanaimba nyimbo za kuabudu, wengine kusifu na kutukuza, wengine tenzi za rohoni. Lakini wote huduma yao ni moja ya uinjilisti. sasa itashangaza mmoja wa kuabudu anamuonea wivu wa kusifu na kutukuza, na wa kusifu ana wivu na wa tenzi za rohoni. Wanasahau kabisa huduma yao ni moja na wote kazi yao ni kurudisha mioyo ya watu kwa Mungu.

ni bora hata waimbaji wa nyimbo za injili, lakini hawa wafundishaji wa neno la Yesu Kristo, wivu umezidi kwa Huduma walizopewa na Roho mtakatifu.
ni kushambuliana tu wakitumia madhabahu walizopewa kwa ajili ya huduma.
Yesu Kristo aliacha huduma TANO kwa kanisa na huduma hizo ni:
1. Utume: mtu mwenye hii huduma huwa hakai sehemu moja ni kuzunguka huku na kule, kuufikisha ujumbe aliopewa na kazi aliyopewa kuifanya hata kama kuna sehemu anapatikana.
2. Nabii: mtu mwenye hii huduma ni Mtu wa Maono, Ndoto na Mafunuo.
watu hawa wamepewa kuona vitu vinavyokuja mbeleni kabla havijatokea na kujua vilivyopita hata kama hakuwa amezaliwa, na kukusaidia namna ya kuepuka ili usiingie pabaya.
3. wachungaji: watu hawa huwa wanapatikana sehemu moja tu. na ukiwa na shida nao ni rahisi kuwapata. wao kazi yao ni kuchunga kundi ambalo tayari analo.
4. wainjilisti: watu hawa ni watu wa maonyo, acha uovu unaofanya la sivyo ni 🔥 moto unaenda kukuchoma kama ambavyo unaenda kumteketeza anaewachochea, ambaye ni satani.
5. Ualimu: watu hawa ni wafundishaji wa NENO la Mungu. kwa undani wake na lengo ni watu kulijua neno la Mungu kiundani na kuirudisha mioyo yao kwa Mungu.

sasa kila mtu anaweza kupewa huduma yake na namna atakavyoitenda, lakini kuna wengine wanapewa zote kulingana na huyo mtu jinsi alivyo.au kutokana na neema aliyo nayo mbele za Mungu, kutokana na Roho mtakatifu apendavyo.
na kila mmoja ni ili kuwajenga watu kwa faida ya Mungu.
sasa nauliza Wivu wa nini, kwa nini usimwambie aliyekupa huduma, akakupa ubunifu zaidi ili huduma uliyopewa izidi kuwa kubwa na kujulikana.
watumishi walio wengi sasa hivi hawamuulizi Mungu, ndio maana huduma zao hazikui na wala hazijulikani. wamebaki kuwashambulia wenzao wachache ambao wanafunga, wanaomba na kukesha milimani kila wakati ili kuisikia sauti ya Mungu kuhusu huduma alizowapa na namna ya kuzitenda.
watumishi wa Mungu badilikeni, kumsema vibaya mtumishi mwenzio hakuifanyi huduma yako uliyopewa kukua.
Acha kumuita binaadamu mwenzako mungu
 
Hivi ndugu Jesus ameshakuwa Yehova?
Mwana, Roho na Baba wameshaungana? Au wengine wame-cease?
 
Kwanini mungu katufanya kuwa watumwa, ili kutafuta nini kwake na huku ingawa, kayaumba yeye??
 
Soma maandiko vema, ni kawaida kunyukana kama mtumishi anakengeuka na kuleta mafundisho potofu
 
Back
Top Bottom