Nawaza siku nikijipata

Nawaza siku nikijipata

Jimny

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
344
Reaction score
849
Haya ndiyo mawazo yangu siku ambayo nitajipata.

1. Siku nikijipata nitahakikisha bi mkubwa namfuta ule moshi na moto wa kutengeneza pombe kali, huku akikimbizana na polisi na mamlaka za serikali ili tupate kuishi na kwenda shule.Bi mkubwa lazima awake kama king'ora cha ambulance [emoji603].

2. Siku nikijipata nitahakikisha naenda kuishi mazingira ambayo mtu akiniulizia au kuhitaji kufika kwangu ni lazima aelekezwe kuwa kufika Kwa Jimny unatakiwa upande kule juu, Yaan nitahakikisha naishi kwenye nyumba hata ya ghorofa moja au ni jenge juu ya kilima, siku nikijipata.

3. Siku nikijipata nitahakikisha namuoa mwanamke ambaye kwa namna moja au nyingine alinipenda au kunionea huruma ila uvumilivu wa kuwa na mimi ukaisha kwasababu nilikuwa sijajipata, nitafanya hivyo kwasababu maumivu ya yeye kuniacha ndiyo yatakuwa petroli kwa upande wangu kukaza ili nijipate.

4. Siku nikijipata nitahakikisha natembea nikiwa nimekaa kwenye BMW yoyote ile ambayo ni SUV kwani tangu nimebalehe mapenzi yangu na gari za namna hii hayajawahi kuisha.

5. Siku nikijipata nitajenga kanisa/msikiti mtaani kwangu na kutoa sadaka kwa wale ambao hawakubahatika kujaliwa kuwa na kikubwa kwa wakati huo, nitapenda watu wangu wamjue Mungu kuliko kitu chochote.

6. Siku nikijipata nitapenda na kushukuru kuwa na idadi ya watoto wasio zidi au kupungua wawili, hii ni kuepusha migogoro na upendeleo kipindi ambacho nitakuwa nimetoweka duniani.

7. Siku nikijipata nitahakikisha career yangu inaiendeleza na kuifanyia kazi kwa asilimia 100 na biashara zangu binafsi zote zitakuwa zinahusiana au zina muunganiko na profession yangu na hii ni siku nitakayojipata.

8. Siku nitakayojipata nitatamani watu wangu wa karibu wafahamu kwamba hela siyo kila kitu ila ni muhimu ihusishwe katika kila kitu,hii ni baada ya kujipata.

Mengine tutaendeleza badae, wewe ambaye still uko kwenye survival mode siku ukijipata utafanya kipi??

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Ukijipata, au ukipata pesa? Pesa sio kila kitu, lakini kila kitu kinahitaji pesa.
 
Tunga wimbo
1.Nikijipata umenipata, tutakula bata
Si tabata tu hata huko msata wafyata
Hatuko familiar, ila tunaweza anzisha familia.
Kwako sitakaidi kama Yona,kwa Joannah wengine sitaona[emoji23].

2.Ni ishukuru jamii kwa kunipa hi forum, nami kwako sitotia fora.
Tuwaepuke wakora penzi letu moto liwatie bakaora.
Ukipata bando njoo , online tuweke mipango
Nilipe kodi pango, nami nipotelee pangoni kwa uzazi wa mpango.....

Nikijipata Joannah utanipata.

3.Wazushi wenye kughushi ndoa, tutawamwagia kopa kifusi.
Wewe mwenye shikopa kwako zitalivunja kopa.
Vijana jamii wakataa ndoa, niko radhi kuzivunja sheria za kataa ndoa nisikutie doa..

[emoji23][emoji23]Oya badae

Back
Top Bottom