Nawaza tu hii kesi (dhidi ya Lissu) huenda ikawa turning point ya mambo mengi Nchini

Nawaza tu hii kesi (dhidi ya Lissu) huenda ikawa turning point ya mambo mengi Nchini

Leo Lissu anatema nondo sana...Leo Lissu anayoyasema ni zaidi ya Ripoti za Tume.

Niseme hivi hata hio Tume iliyoundwa itakayoyaleta hayatafanyiwa kazi bali haya ya Lissu.

Lissu leo anaonyesha ubovu wa muundo wa utoaji haki,
Vyombo vya usalama,
Vyombo vya kusimamia uchaguzi
Na utumiaji vibaya mamlaka.

Naamini hakuna Mwana Ccm anaesikia haya ya leo akatoa kichwa.

Hakuna kitu kinatokea kwa bahati mbaya....ngoja tuende na hii safari yao mpaka mwisho wake. Kuna atakayeshinda na atakayepoteza.

Muda utaamua hayo
 
Kwanza watengeneza kesi naamini kabisa mpaka kufikia muda huu wanajiuliza imefikaje huku?

Walijua kwa mazoea watamuweka ndani muda ukifika wamwambie fanya hivi na vile atii, kisha wamuachie.

Ghafla ndio wanashangaa jamaa hawaelewi, kila wakimpa condition ili wamuachie badala atii, nae anawajibu kwa kuwapa condition!.
 
Leo nimefuatilia kesi ya LISSU kuanzia alifu mbaya wasalamu, na nimepata picha kwamba taifa letu linapaswa kupata katiba mpya yenye mamlaka ya usimamizi wa misingi yake, maana kitu kikubwa kabisa hapa ni kwamba misingi ya haki, demokrasia za kisiasa, utawala bora na utawala wa sheria vimeifadhiwa kwenye mamlaka ya mwenye maslahi ya kisiasa, kiukweli mayai haya hayapaswi kuwekwa kapu moja kamwe, Yaani mwenye maslahi ya kisisasa hawezi kamwe kuwa msimamizi wa misingi ya demokrasia ya kisiasa, Baada ya kusema haya naomba nipendekeze kwenu "Rasimu ya katiba yenye muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa", Yaani.

1. Baraza la usimamizi wa taifa;
Baraza hili ni muhimili wa usimamizi wa misingi yote ya kitaifa, mamlaka ya kimuungano, tathmini za kitaifa na muungozo kwa hali ya taifa pale Kanuni za ulinganigu wa nguvu za kikatiba zinapoingia.

2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania; serikali ni muhimili wa utendaji, utekelezaji wa sera za serikali na taifa, ulinzi wa taifa na mengineyo kama rasimu hiyo itamkavyo.

3. Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania; bunge ni muhimili wa uwakilishi wa wananchi wenye jukumu la kutunga sheria, kupitisha bajeti za taifa, majadiriano ya muelwkwo wa taifa na mengineyo kama rasimu yenyewe itamkavyo.

4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa Tanzania; Mahakama ni muhimili wa utoaji haki, mfasiri wa katiba na sheria za nchi, mtoa huku wa makosa ya jinai na madai na mengineyo kama rasimu yenyewe itamkavyo. Jambo la kipekee ni kwamba ndani ya muhimili huu kuna mahakama ya katiba yenye mamlaka ya juu na ya mwisho kabisa ya mashauri ya kikatiba nchini.

Muundo huu unahakikisha uwajibikaji, uwazi, uadilifu na kuondoa kabisa ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma na mwisho kuibua usawa na mshikamano wa kitaifa.

katika rasimu hiyo inayopatikana katika tovuti ya www.katibampya.com Mihimili hii yote minne imetamkwa kwenye SURA YA NNE ya katiba hiyo kwa kuanza na Baraza ibara ya 98 mbaka ibara ya 116 kisha kuendelea mihimili mingineyo kwa mpangilio wa nambafi kama ulivyoweka hapo juu.

Aidha pia Sehemu kubwa ya historia ya LISSU imezungumzia Uchaguzi, na niendelee kusema kwamba Rasimu ya katiba kwenye tovuti tajwa haijaishia pekee kwenye Kuanzisha Tume huru ya uchaguzi, katika ibara ya 212, rasimu hiyo emeenda mbali mbaka kuanzisha, "Mchakato wa uthibitisho wa uhalali wa madaraka na kupingwa kwake" katika ibara ya 176.

Embu fikiria Kabra ya kuapishwa kwa Rais, mbunge na Diwani Kuna mchakato Maalumu wa kikatiba wa kuthibitisha Kura, ushindi na hapo ndipo Mahakama ya katiba inaitisha Uhapisho rasmi, Zoezi hilo limewekwa kwa muda wa siku 30 mbaka 73 pekee.

Haya yote ninayoyasema hapa si maneno ya jumla hivyo ni wajibu wako kufika kwenye tovuti hiyo na kusoma rasimu hiyo hasa kuanzia kwenye ibara nilizozitaja hapo juu au kuanza mwanzo hadi mwisho.

Angalizo; Rasimu hiyo ya katiba haiondoa mchakato rasmi wa katiba, Hivyo basi Rasimu hiyo ni maoni ya kisomi, kitaaluma yanayoitaji jicho la kisomi, kitaaluma na raia wote kwa ujumla na kwa maoni haya nina imani pale mchakato rasmi utakapoanza basi Wananchi wote tutakuwa na taswira nzuri ya nini kilicho bora.

chanzo: www.katibampya.com
 
Aliyekuwa mgombea wetu wa Jimbo la Mrimba, anaitwa Suzan Kiwanga wa Mrimba, anarudisha fomu, akakuta Mkurugenzi kafunga ofisi, hayupo.

Ilipofika saa 11, Mkurugenzi kajitokeza, kasema, “Umechelewa, Mama,” na mgombea wa CCM kapita bila kupingwa.
 
Lissu ameibua hoja ya msingi , namnukuu

"Ukiangalia chaguzi za kabla ya mwaka 2020 Tume huwa zina gazette matokeo yote jimbo kwa jimbo na Kata kwa kata nchi nzima.

Ya Ubunge Jimbo kwa Jimbo nchi nzima lakini ya Urais huwezi kuona kokote kule.

The results were never gazetted na sheria inasema baada ya miezi 6 yatachomwa moto. Hatutakuja kujua Magufuli alipata kura ngapi? Kwanini? kwasababu Tume ni ya KiCCM. "

Hii imeendelea hata igizo la mwaka jana tuliloambiwa ni uchaguzi 2025 hakuna matokeo katika tovuti ya tume tunayoambiwa ni huru.
 
Leo Lissu anatema nondo sana...Leo Lissu anayoyasema ni zaidi ya Ripoti za Tume.

Niseme hivi hata hio Tume iliyoundwa itakayoyaleta hayatafanyiwa kazi bali haya ya Lissu.

Lissu leo anaonyesha ubovu wa muundo wa utoaji haki,
Vyombo vya usalama,
Vyombo vya kusimamia uchaguzi
Na utumiaji vibaya mamlaka.

Naamini hakuna Mwana Ccm anaesikia haya ya leo akatoa kichwa.
Tanzania haiwezi kuendelea kama ilivyo sasa. Ni lazima mabadiliko yawepo. Haya hayakwepeki tena.

Tanzania will never be the same again.
 
Back
Top Bottom