Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Wakuu kwema?
Leo Timu ya Simba SC inafanya uchaguzi wake wa Mwenyekiti wa Timu kupitia wanachama na pia Nafasi ya Wajumbe watano kuingia kwenye Board.
Katika wagombea wa nafasi ya Uenyekiti kupitia Wanachamna ni pamoja na Bwana Murtaza Mangungu ambae ndie Mwenyekiti anaemaliza muda wake. Huyu Bwana ni Kada na Kiongozi maarufu tu katika CCM akiwa pia amehudumu pia kama Mbunge kupitia chama hicho.
CCM imekua ikishinda uchaguzi kupitia mbinu mbalimbali tu ambazo nyinginezo hua zinakua za nje ya sanduku la kura (sizitaji). Tumekua tukiingia kwenye chaguzi ambazo zinahusisha CCM na kua kama tunakamilisha tu ratiba sababu mechi inakua ishachezwa kitambo tu.
Murtaza Mangungu kama mwana CCM kindakindaki ni wazi anazijua mbinu hizi. Hapa ni wazi kua Wakili Msomi Kaluwa kutoboa ni ngumu sana karibia na haiwezekani. Labda kwa Wajumbe kidogo kutakua na fairness lakini sio kwa nafasi ya Mwenyekiti.
Nawasilisha,
Jumapili Njema