Hiyo miaka hela yetu itakuwa imeshuka thamani ... Hili nalo mkalitazame
Hendi kuifungia hiyo 100 anaenda kuiwekeza maana yake inazalisha.. sasa Kama atapata 10% kila mwaka na inflation kwa mwaka hata ikiwa 5% hapo huoni kama imelinda thaman ya pesa yake
Ingekuwa anaenda kuifungia bila kuzalishwa ndio ungesema thamani ya pesa inashuka . Kuiwekeza pia ni kama kufanya biashara hivi sijui kwa nini mnachukulia kama kuwekeza ni kama kuweka akiba..
Mfano alie na mtaji wa 100m na akafanya biashara ya kuuza nguo ambayo inampa 1m kwa mwez kwenye mapato hana tofauti na aliewekaza UTT au Govt Bond maana nae atapata almost the same
Tofauti yao huyu wa biashara ya nguo anaweza akapata zaid au akapoteza zaidi. Inategemea na aina ya biashara ( the high the risk the high the returns) huyo wa UTT atakuwa na almost fixed faida kila mwaka sababu risk ni ndogo
Kuwekeza kwenye UTT sio kama unaiweka fedha bank eti itashuka thaman kama ingekuwa haizalishi sawa, pale unafanya boashara pia.. yaan wewe ukiwekeza kwenye masoko ya hisa na mitaji ama hizi MMF unafanya biashara pale .. wale kina Mr. Kuku au wale jamaa wa kilimo sijui wekeza kwenye shamba tunakulimia na kukutafutia wateja.. utaona Bussiness model yao haina tofauti na UTT maana yake unawapa fedha yako wanaifanyia biashara wanakupa faida kiufupi na wewe unafanya biashara ya kilimo pia sio lazima ukifanya biashara flan uwe front.
Pia Tunaposema pesa inashuka thaman maana yake kitu cha 15m sasa hivi baada ya miaka 10 utakinunua kwa labda 30m , sasa kama mtu kawekeza 15m baada ya miaka kumi akawa na 30m maana yake bado ana uwezo wa kukimudu kukinunua.. tofauti na yule alieiweka tu hiyo 15m isizalishe maana yake atalazimika kuitafuta 15m ingine ili aweze kumudu hicho kitu.. huo ndio msingi wa kusema pesa imeshuka thaman
Ingekuwa uwekezaji wa UTT haulindi thamani ya pesa ingekuwa haina maana.. UTT inakupa passive income maana yake pesa yako iko sehemu inazalisha na bado una uhuru wa kufanya jambo lingine mfano kama ni mwajiriwa.. ukiwekeza kwenye biashara inayotaka mda wako kila siku hiyo maana yake una uhuru mchache wa kufanya jambo lingine.. ndio maana inaitwa active income.. sababu ili pesa izalishe faida ni lazima pia uwekeza na mda yaani ushiriki kwenye mchakato mzima uwekezaji wako ni wa Fedha na mda 100%
Mfano mimi nauza magodoro mana huyo jamaa
OgaBoy akasema nakupa 100m uwe unanipa 1m kila mwaka.. maana yake mimi kila siku na deal na supplier na deal na wasafirishaji pia na deal na wateja.. yaan hapo mda wangu unatakiwa kila siku.. maana yake kitendo cha siku kuw anje ya biashara kinaikuza risk mwisho wa siku ikiwa tumepata faida labda 2m atachukua 1m yake.. pamoja.na kuwa utaona tumegawana faida 1m kila mtu.. alichonizidi yeye ana mda wa kufanya mengine ya kuingiza kipato zaidi maana yake hii biashara ya magodoro kwake inampa passive income mie inanipa active income
Ndio maana waswahili wanasema tajiri na mali zake.. maana mtu tajiri lakini utajiri unamfanya mtumwa.. sababu ni lazima ashiriki kikamilifu kwenye biashara ili asipate hasara kitendo cha kuwa na off day isiyo na mpangilio kinampa Risk ya kupata hasara
Ndio maana unaona ki bongo bongo mara nyingi familia na watoto ndo watafaidi matunda manaa baba unakuwa always busy..