Nawekezaje bumu linisaidie kulipa ada?

Tena wanafunzi wengi wanakula cafeteria za vyuoni kwao kwa sababu bei chee au wanapika maghetoni kwao.

Kwa hiyo akiingia hiyo biashara ana asilimia kubwa ya kufeli.
Kweli kabisa. Mi sishauri kabisa mtu ajiingize kwenye biashara.
Mybe mda wa likizo ajue anafanya nini ila sio kama hawa wanaotoa ushauri wa ajabu.
Asilimia nyingi wanao ongea wapo mbali na mazingira ya chuo au walipitaga miaka hiyo.
Hawajui now mambo yamebadilika sana
 
Huko mavyuoni kwao hiyo migahawa imejazana ,akiingia kwenye hiyo biashara ataangukia pua.
Mkuu,katika biashara na ujasiriamali regardless of where kuangukia PUA huwa kupo.Ila huwezi kuangukia PUA just Because umeanzisha Biashara Chuoni n tayari kuna aina hiyo ya Biashara.Siku hizi biashara inahitaji Ubunifu kidogo kisha mambo mengine yanaendelea...
 
Kuingia kwenye biashara,utalia km home ni bush au Kuna nafasi home na mtu wa kueleweka fuga zako tu ukitoka uyajua pa kuanzia,Ila Mambo ya frem sijui leseni itakulamba
 
Inategemea na biashara mkuu ukiweza kubalance coursework na biashara mambo zinaenda hata ukijamaliza una uzoevu mkubwa

Naongea kutokana na uzoefu
 
Ushauri wangu tafuta mtu wa karibu ambae kwa namna moja au nyingine mnasaidiana katika kupambana na life iwe kaka yako, dada yako au rafiki yako wa ukweli(iwe life mnasongesha pamoja) ambae yeye kajikita kwenye biashara toka zamani wekeza nae uwe unamuezesha mtaji huku mkipanga mipango ya baadae unaweza pata backup ya ada au matumizi mengine huku mipango ikiendelea

Kufanya mwenyewe inaweza kuwa ngumu kidogo kwakuwa mwanzo ni mgumu ila ukipata mbereko inakuwa vizuri
 
kuna mradi watu wanaudharau sana ila una hela nao si mwingine bali ni shoe shine
na shoe repair.
Unapata site na kuweka vijiwe vitatu hadi vinne, unanunua mahitaji yote unampa
fundi,huyo kijana wako, unapatana naye malipo kwa siku.
Na ukibahatika ukapata kijiwe hapo chuoni itakuwa poa sana.
Unawapitia kila siku jioni kukusanya mapato au kama ni waaminifu wanakuwekea kwenye simu.
 
Hizo fursa ni zipi tupe Sisi wenye kozi rahisi za miaka mitatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…