Naweza fanya biashara gani kwa mtaji wa 15m?

Kama unaweza kufanya kuinvest project ya kuanzia mwaka 1 mpaka mmoja na nusu na ukasahau umaskini maishani mwako nicheki PM. Ni uhakika na haina hasara mkuu.

Kwa nini usiwe muwazi ili members wengine nao wafaidike na ushauri wako!!!
 
Hii kitu Napenda sana...taratibu za kuianzisha Napenda kujua zimekaaje? Kuna Uzi humu uliwahi kuongelea hii kitu ila siukumbuki
 
Kama unaweza kufanya kuinvest project ya kuanzia mwaka 1 mpaka mmoja na nusu na ukasahau umaskini maishani mwako nicheki PM. Ni uhakika na haina hasara mkuu.
Pm huko kuna nn funguka hadharani kila mtu ajifunze, namuasa jamaa awe makini na matapeli maana wengine wanatolea macho pesa ambazo c zao
 
Fungus ofis za M-PESA Tigo,aitel na Nmb Wakala uza vocha sajili line na vifaa vya simu kama betri,kava weka na gas za matumizi ya nyumbani etc mm npo huko miaka 6 sasa kwa ushauri zaidi call 0764616353 for free
 
Ila inategemea upon mkoa gan wish u all ze best kana we ni mfanyakazi wa serkalicau kampun binafsi itakugharimu sana kwenye usimsmamizi wa biashara ila kama upon na shemej everything will be fine
 
Fungus ofis za M-PESA Tigo,aitel na Nmb Wakala uza vocha sajili line na vifaa vya simu kama betri,kava weka na gas za matumizi ya nyumbani etc mm npo huko miaka 6 sasa kwa ushauri zaidi call 0764616353 for free
Electronic money transfer pamoja na vocha za jumla na si rejereja ,akipata site nzuri mwaka mmoja anaendesha Audi q6 ,hizo gesi sijui kusajili laini uchawi tu kwa milion 15.
 
Vitu vingine vina mutual benefit. You win, I win. Kqtika mazingira kama haya ni ngumu kumwaga kila kitu. Ila ukitaka nikumwagie wewe nifate PM. Kuwa na amani
Mkuu mie nimwagie PM...win win situation guarantee
 
Hiyo idea ya laki tatu inaweza watoa watanzania wengi mkuu, hebu share nasi hiyo kitu.
Kuna MwanaJF alitoa ushauri, ulionukuliwa hapa chini. Nami nasisitiza kuwa yawezekana na faida yake ni kubwa, baada ya miezi sita (6).

Ikumbukwe kuwa ujenzi wa viwanda, hasa vya kuonfeza thamani ya mazao ghafi, ni fursa kubwa ya kujihusisha na uzalishaji mazao ya biashara na chakula.

Kwa mfano, viwanda vya kusindika nyama ya ng'ombe, kitoweo kikubwa kwa wakazi wa mijini, kunatoa fursa ya kukua kwa ufugaji wa kuku, maana nyama ya kusindikwa ni kwa soko la nje, na bei ya nyama ghafi ikaongezeja bei, hivyo kuruhusu kukua kwa soko la nyama ya kuku.

Isitoshe, mfugaji wa kuku akiweza kuweka na bwawa la samaki, anakamilisha mnyororo wa uzalishaji. Kuku watampatia mbolea kwa ajili ya kurutubisha bwawa la samaki. Maji ya bwawa yatampa maji ya kumwagilia bustani. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku, samaki na bustani, hakika ni pato tosha la kuondokana na umaskini.

TAHADHALI NI LAZIMA UTUMIE WATAALAMU KWA SHUGHULI HIZO ZA UZALISHAJI.

Nukuu:

"MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.

Hapa utahitaji kuku 11 tu wakubwa wanaotaga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu (300) au na zaidi kama unataka.

Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.Tafuta sehemu ya uhakika na nunua kuku wenye matunzo na kinga ili wasipatwe na magonjwa na wenye afya nzuri.

Unaponunua kuku wakubwa kwanza unapowafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.

Usinunue kuku kabla hujaandaa banda la kutosha kulingana na idadi ya kuku na kwa ajili ya badae kwa kuwa mradi utaongezeka kadri siku zinavyoenda na Chakula.

Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

Mchanganuo Wa 69500 ni:-
1) Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.<
2) Paraza (mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku) kilo 25 = 700x25 =17500.
3) Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
3) Layer's concetrate, Kilo 25 kifuko. = 21500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi - Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku: Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300. Hivyo tutaweza kuona Chakula hicho kitakupeleka zaidi ya siku 100 au zaidi ya miezi mitatu.

Kwa laki 3 utabakiza 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU, na mchanganuo wake ni: Kwa kila kuku mzuri ambaye hajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000 - Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.

Itakuwa imebaki shs. 60500 kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20.

Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga

Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.

Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000. Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200.

Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Kwa maana kwamba kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kuku hao wanakuingizia 120,000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia, hivyo utachanganya Chakula cha aina moja tu, kwa kuwa wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.

Kumbuka kujibana ili kuongeza ukubwa wa banda"
 
Kuna biashara ya kuku ambayo inaendelea kwa mjini mwanza ambapo wale jamaa wa *kuku poa* wanakupa vifaranga na chakula cha kuku .yaan mtaji wako wewe inakuwa ni mabanda tu.ila sharti yaweze kuweka zaidi ya kuku 5000, wanapita kukagua mara mbili kwa wik then ikiisha wiki tano wanakuja kuchukua kuku wao na kukulipa 1000 kwa kila kuku,
So kwa pesa uliyonayo unaweza tenga fungu ata ukaweka mabanda ya kubeba kuku 10000. Na baada ya wik tano ukawa na uhakika wa 10000*1000=10,000,000/=
Kwa maelezo zaid fika ofisi za kuku poa pale mwanza
 
Toa "address" yao
 
duh nakwenda pale kesho tu asbh mapema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…