Usianzie mbali 20k ni kubwa mno ,anza mdogo mdogo ,nenda viwandani ,kuna kazi za kike za kuweka label kwenye machupa ,omba kazi kwenye migawaha sehemu zilizochangamka ,omba kazi za call cntre ,wauza line ,usajili line etc unapofanya movement hapo ndipo unajenga connection.
Mimi baada ya kumaliza elimu ,nilianza na kazi ya ukuli ,kupakia chupa za soda na kuepeleka kwa wateja ,kuna siku tukapeleka kwenye Duka la chuo nilichosoma na nikashusha kafteria halafu kuna nyomi la vijana niliowaacha chuo wanakucheck.
Ukimaliza unalipwa Tsh 2000 tena kesho yake ,hiyo ni miaka zaidi ya 20 iliyopita ,daladala ilikuwa Tsh 100 au 150.