sipati unatokeza kwenye kichaka na jembe lako....
halafu huyoo kwenye lap top yako unakuja kuchangia mada jf.....lol
jamani siwezi kujenga nyumba ya vyumba vinne hapo dar kwa milioni 20????niambieni kama siwezi kabla sijaipoteza hii pesa...
Thanks,
Kwa kuwa kiwanja unacho millioni 20 mbona unahamia kwenye nyumba lakini finishing hutamaliza. Angalia mgawanyo wa gharama ( I assume uko Dar es Salaam na nyumba unayojenga ni ya mtu anayejenga nyumba yake ya kwanza):
- Matofali 5,000 @700=TZS3,500,000
- Mafundi (kujenga toka msingi mpaka kuezeka)=4,000,000/=
- Cement mifuko 150 @15,000=2,250,000/=
- Mbao zote TZS4,000,000/=
- Bati 60 @ 15,000=900,000/=
- Fundi umeme na vifaa vyake=5,000,000/=
- Finishing (madirisha na milango)=5,000,000/=
- Finishing (plastering + ceiling works)=5,000,000/=
Exactly.. Akiondoa gharama za msingi pengine million 20 inaweza labda kutosha, #justsaying
mkuu hapo namba5, na 7 hivi hizo bati unazoziongelea kwa laki9 ni zipi au madirisha na mirango yepi? Mi binafsi nimeupitia mchakato huo na kwa nyumba ya vyumba vi4 labda twaweza kutofautiana size ya madirisha lakini magrili zilinitoka m3.4 na aluminiums m4.3 total m7.7 na upande wa bati nilitumia zile za versatile bati tuu niliwaachia alaf kiasi cha m5.2 hapo hujazungumzia misumali wala mbao. Nadhani angeweka wazi nyumba ya aina gani
anza kujenga achana na paper work nyumba hujengwa mdo mdogo si kwa siku moja au wiki wewe si fisadi bana.
Fyi- nunua matofari ya foundation, kokoto, mchanga na nondo. Ongea na fundi atakujengea sh.ngapi foundation! Akimaliza foundation elewana naye toka hapo hadi kwenye lintre baada ya hapo lintre then anamalizia.
Mafundi si waaminifu aise.
Unaweza kujenga na ikabaki,
hebu ni pm kama uko serious..
I likes positive minds like this..., it's good to be opportunistic rather than having pessimistic mind..
wakuu kwa kiasi icho nikaamua kujenga kule kijijini kwnagu moshi inatosha?asume kiwanja kipo flat level...matofali ya kuchoma....nyumba iwe ni ya kawaida ie. vyumba vitatu vya kawaida,choo cha public ndani,sehemu ya jiko,dining labda na sebule.mnasemaje wataalamu
thanks wote kwa michango yenu,mliosema haitoshi mbona hamjasema ni shilingi ngapi ndio inatosha?lol anyway thanks nimeona nisijenge sasa hivi...mpaka nikiwa na hela lol
thanks wote kwa michango yenu,mliosema haitoshi mbona hamjasema ni shilingi ngapi ndio inatosha?lol anyway thanks nimeona nisijenge sasa hivi...mpaka nikiwa na hela lol
Unajua Abd. watu wengi wanapenda tu kusema nikiwa na shillingi kadhaa naweza fanya hiki? Ukweli ni kama yawezekana,lakini ujenzi ni fani kama fani nyingine kama vile utabibu,uwanasheria na kadhalika!
Nimekua kwenye industry ya kujenga kama mtaalamu na pia kama mjasiliamali kwa gd number of yrs,pamoja na pesa watu huwa wanasahau kitu cha muhimu kabisa na basic nacho tunakiita
Conception stage hii ni stage ambayo muhimu na ambayo anaetaka kujenga anatakiwa atoe idea yake nini anataka na kiwe wapi kulingana na mahitaji yake,bila hata ya kuenda stage nyingine wataalamu tutamshauri na kumwambia pesa inatosha au la!
Jamani is a professional thing!
Tunaamini kila mtu aweza kujenga lakini mtaaalum atajenga kwenye reasonable cost na acceptable quality!
Good day!