Kifimbocheza
JF-Expert Member
- Aug 7, 2008
- 494
- 121
Mbona hujaweka NONDO
Nondo mm12 ni Tzs 19,500 kwa Nondo Moja
Nondo mm12 ni Tzs 19,500 kwa Nondo Moja
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna Quantity Surveyor wa kutosha na wenye rekodi njema ya kazi hapa mjini na wanaweza kukupa mwongozo wa jinsi ya kujenga kwa kiasi ulichonacho... na siku hizi teknolojia ya uujenzi wa gharama nafuu inazidi kuongezeka....jamani siwezi kujenga nyumba ya vyumba vinne hapo dar kwa milioni 20????niambieni kama siwezi kabla sijaipoteza hii pesa...
thanks,
Kwa fundi mie huwezi......labda fundi mwengine :[
Google ''low cost house plans''
Haukuwa na haja ya kujenga sis getruda,kama unacho kiwanja hela yako inatosha kabsa na hata kama hauna kiwanja viwanja vipo vya kuanzia mil 1 mpaka 6,na hiyo 14 itamalizia mpaka unahamia ni pm nikupe michongo yote hadi una maliza nyuma yako,ya kisasa kabisa.
Wee acha kukata tamaa mbona 20m inatosha nyumba pamoja na kausafiri kako kabisa, mie nimepanga nyumba isizidi 10m naitakua kubwa nzuri ya kupendeza, humu jf watu wamezoea kuwadiscourage wenzao, wao hawana hata vibanda wathanks wote kwa michango yenu,mliosema haitoshi mbona hamjasema ni shilingi ngapi ndio inatosha?lol anyway thanks nimeona nisijenge sasa hivi...mpaka nikiwa na hela lol
Mimi ningekuwa wewe wala nisingeanza kupanga mipango ya kujenga nyumba. Ningeanza biashara ya kusafirisha nguruwe kwa mchanganuo huu hapa chini
1. Nguruwe 150 wadogo @ 10,000
2.Chakula (mashudu) Tshs 5,000 kwa mwezi kwa nguruwe mmoja
3.Ujenzi wa mabanda Tshs 250,000
4.Mlinzi Tshs 20,000 kwa mwezi
5.Matibabu Tshs 30,000 kwa mwezi.
Nguruwe huchukua miezi 6-8 kwabla ya kuanza kuuzwa. Kwakweli ni biashara nzuri sana na ndani ya miaka miwili unaweza kuwa na hela chafu kiasi cha kugombewa na mademu kama mpira wa kona.
vyumba vinne means one bed room, sebule moja, jiko na stoo moja na choo kimoja. ila vyote vinakuwa ndani
chumba kimoja cha msingi wa kozi tatu ni matofari 300 * 4 = 1200
au kozi tano ni matofari 500 * 4= 2000
maximum tofari 3000/50 = 60 mifuko ya cement. * 14000= 840,000
mafundi matofali + mchanga + machine+ kumwagilia= 900,000
fundi kujenga mpaka linta + kupiga linta na kuinua kozi za juu= 2,000,000
fundi kuezeka 600,000
mbao treated ( inategemea na design) maximum= 1,000,000
bati 28 geji 120 * 160,000= 2,300,000
dirisha moja 240000 * 10 = 2,400,000
milango 7 * 150,000= 1,050,000
kupiga ripu fundi + cement + mchanga = 800,000( ndani) + 800,000 ( nje)
gypsum = 60 * 14,000= 840,000
fundi gypsum + rangi= 600,000
tyles nyumba yote = 1,500,000
fundi tiles= 500,000
wiring vifaa= 1,500,000
fundi wiringi = 600000
pigeni jumla ni ngapi haya ni mahesabu ya juu sana
Hii hapa
![]()
Ila Umesahau Plumbing and Sanitary Works..Tiles etcKwa kuwa kiwanja unacho millioni 20 mbona unahamia kwenye nyumba lakini finishing hutamaliza. Angalia mgawanyo wa gharama ( I assume uko Dar es Salaam na nyumba unayojenga ni ya mtu anayejenga nyumba yake ya kwanza):
- Matofali 5,000 @700=TZS3,500,000
- Mafundi (kujenga toka msingi mpaka kuezeka)=4,000,000/=
- Cement mifuko 150 @15,000=2,250,000/=
- Mbao zote TZS4,000,000/=
- Bati 60 @ 15,000=900,000/=
- Fundi umeme na vifaa vyake=5,000,000/=
- Finishing (madirisha na milango)=5,000,000/=
- Finishing (plastering + ceiling works)=5,000,000/=