Naweza kumbadilisha aache kuvuta bangi?

Naweza kumbadilisha aache kuvuta bangi?

odamae

Senior Member
Joined
Nov 5, 2020
Posts
163
Reaction score
291
Kuna mwanaume ananipenda sana naona tuna match dini na umri japo umri tumepishana mwaka 1 Mimi nimemzidi.

Shida anavuta bhangi sijui ni mkumbo ila ni mpole mstaarabu. Naweza kumrekebisha au niachane nae tu? Inafika muda najikuta kama namuogopa hivi.

Hakuwahi nambia kama anavuta ila nilizikuta kwenye room yake ambazo zishatumika.
 
Yaani sijui lini watu mtakuja kugundua kwamba bhangi haina uhusiano na ukorofi, wizi, ukibaka, ugomvi n.k.

Sista, asilimia kubwa ya wanaovuta bhangi ni wastaarabu kinoma. Ukweli nakuambia.

Tatizo ni poda. Uko ukianza hauchomoi na unapotea mazima.

Mpe nafasi mshikaji, huwezi jua alianza kwanini, yaan unataka umpoteze soul mate kisa cha kitoto hivo. Give a try madam. All the best.
 
Mad Max, yawezekana dada haipendi bhangi! pamoja na kuwa unaona haina kasoro
 
Yaani sijui lini watu mtakuja kugundua kwamba bhangi haina uhusiano na ukorofi, wizi, ukibaka, ugomvi n.k.

Sista, asilimia kubwa ya wanaovuta bhangi ni wastaarabu kinoma. Ukweli nakuambia.

Tatizo ni poda. Uko ukianza hauchomoi na unapotea mazima.

Mpe nafasi mshikaji, huwezi jua alianza kwanini, yaan unataka umpoteze soul mate kisa cha kitoto hivo. Give a try madam. All the best.
Wewe unavuta bila shaka
 
Huwezi kumrekebisha! Hiyo ndio tabia yake. Chagua mwenyewe kutokana na umri wako kama unapass time sawa. Vinginevyo unataka Baba wa watoto mvuta bangi? Maana tabia itazidi akipata stress za ndoa
 
Bhange sio issue kama anatimiza majukumu yake mengine bila tatizo. Wavuta bhange ni wengi na ni watu wastaarabu na wanareson kwa hekima.

Ni kwakuwa tu inakatazwa lakinini amini nakuambia ukizunguka nyuma ya pazia unaweza kwakuwa usio watarajia wakivuta bhange, hasa wanasiasa na wataalamu mbalimbali.

Mfano kuna marais kibao wanavuta hii kitu kama yule wa Kenya inasemekana na hata yule alieondokazake ninawasiwasi. Kama unampenda upende alivyo kuvuta bhange sio udhaifu wala sio uhodari
 
Wavuta sigara ni wamoja wakifuwatiwa na wavuta bangi sijawai ona apa duniani
 
Vijana Mkiwa kwenye Mahusiano hapo ndio pakujuwa Mbichi na Mbivu za muelekeo wa Maisha yenu ya Ndoa..,
Hv Leo kwenye Mahusiano unaishi kwa hofu je hiyo hofu utaweza kuishi nayo kwenye maisha yenu yote ya Ndoa?
Ndoa nyingi zinavunjika kutoka na Maisha ya Kisanii wanayoishi katika hatua ya Uchumba, haliyakuwa ukiingia kwenye Ndoa unahitaji kuishi uhalisia wako lazima Ndoa iwe ngumu..,
Lamsingi hakikisha mnaoneshana uhalisia kuanzia kwenye Uchumba, hilo litasaidia hata mkiingia kwenye Ndoa kusiwe na kusema huyu amebadilika!
Kumbuka Tabia usiyo ipenda Leo inaweza kuongezeka ama kupungua kwenye Maisha ya Ndoa hivyo malizaneni kwenye hatua ya Uchumba ili mbivu na mbichi zionekane kabla hamjaingia kwenye Ndoa!!!
 
'sirikali' iko mbioni kuihalalisha, hakuna shida mtu kuvuta bangi

big NO, huwezi mbadili
 
Back
Top Bottom