Mahengeson
New Member
- Jul 17, 2011
- 3
- 0
Uwezo wa wazungu unatokana na fursa wanayopata ya kujua mambo mengi in general. Mfano, Mwafrika wa kawaida anaweza akawa na akili sana lakini hajui kutumia computer au kupata nafasi ya kuyafahamu mambo mbali mbali ya kidunia kupitia Internet, magazeti na kusoma vitabu sana. Hii inatokana na mifumo yetu ya elimu na pia tunakokulia. Tofauti na hivyo, Wazungu, in general wana opportunity kubwa ya kupata vitabu au kutumia internet tangu wakiwa wadogo kabisa na hivyo kujua mambo mengi akiwa bado mdogo. Mimi nadhani Waafrika tuna uwezo mkubwa wa kufikiri kama wao ila tunachokosa ni fursa. Pia, uwezo wa kufikiri unaweza kuongezeka kama kwanza utakubali madhaifu yako na nguvu zako kisha kufikiri positively. Ukizidi kufikiri kushindwa, utashindwa na kama utafikiri mafanikio, utafanikiwa. Labda cha muhimu ni kufanya mazowezi ya mara kwa mara ya kufikiri na hii inasaidiwa kwa kushiriki katika mijadala kama wenzangu walivyosema. Mada au kufikiri kwako lazima ujitahidi kuendane na umri wako au zaidi.