Naweza kuongeza uwezo wa kufikiri?

Naweza kuongeza uwezo wa kufikiri?

Hapo ndy naanza kupata mashaka na uwezo wako wa kufikiri!

Nafikiri inawezekana kabisa wewe ndiyo ukawa na matatizo ktk uwezo wako wa kufikiri. Unataka kukimbia ukweli.

Rosemarie amejaribu kujitathmini akagundua mapungufu, anatafuta msaada ili awe bora. Kuonyesha uwezo wake kufikiri ulivyojuu ametambua kuwa kiini cha mapungufu ni namna anavyofikiri; hakusema ni kwasababu hana kitu fulani. Perfect evaluation. Huwezi kufanya kwa ubora hata kama tukikupa kila kitu lakini uwezo wako wa kufikiri ukiwa chini.
Amefanya kazi na wazungu akaiona tofauti aliyoandika. Ni mkweli. Hujamjibu umemshambulia kwa kushuku uwezo wake wa kufikiri. Si vema.

Kiukweli Rosemarie, unaweza ukafikiri sahihi kwa kiwango kikubwa kupita wanaume wa umri wako. Tena unawezakufikiri kupita wazungu. Ngoja tusubiri inputs za Invisible. Lakini nitachangia machache: ya kuwa vikwazo vingi vipo ktk namna tunavyolelewa na vingine vipo ndani yetu. Katika malezi tunayolelewa/tuliyolelewa
1. Hayatufundishi kuthubutu bali woga
2. Hayatufundishi kujiamini bali kuwa tegemezi
3. Hayatufundishi kuona kosa ni fursa ya kujifunza bali ndiyo mwisho (kushindwa)
4. Hayatufundishi kuitambua na kuithamini kazi ndogo/mafanikio madogo kuwa ni mtaji wa kutuchochea kufanya makubwa.
5. Hutufundisha kuona kufanya kazi kuwa ni utumwa wakati kazi ni utoshelevu wa maisha ya mwanadamu.
6. Hutufundisha kuona kuwa sisi hatuwezi ila wao/yeye anaweza, na wakati kuwa hata yeye hawezi kamwe.
Orodha ni ndefu.

Wengi wa wazungu tunaowaona kuwa ni bora ni kwasababu ya uzoefu, exposure, uthubutu na kujiamini. Ukifanyakazi hata na mtanzania aliyekuzidi katika eneo lolote ktk hayo mengine mko sawa mara zote utamwona bora .

Nitarudi.
 
1. Reading
2. Reading
3. Reading
Note: important stuff zaidi,ukijikita kwa kina shigongo utakuwa hivyo hivyo,kishigongo shigongo
Hongera kwa kutafuta kukuza maarifa!

Karudie kusoma, shida yake si kutafuta kukuza maarifa.

Shida yake ni kujua kama kuna-uwezekano wa kuongeza uwezo wa kufikiri. Na ikiwa kama upo ni kwa namna gani afanye ili aongeze?
 
Nimegundua kitu kimoja:

Ukitaka kuongeza uwezo wa kufikiri kuna hizi njia ambazo zitweza kwa mtu kujaribu kuongeza uwezo wa kufikiri (kwa ninavyojua mimi lakini!)

1. Vyakula vyenye wingi wa madini ya zinc na calcium.
2. Kujiunga katika kushiriki katika challenges mbalimbali za kimaisha(kwa mfano: Kitu ambacho hujawahi kukiona au kukifahamu jaribu kifahamu vizuri maana hapo inakuwa kama shule mpya kwako, wazungu hili wanalo sana we angalia wanavyosfiri na kuwaonesha mambo mbali mbali kwa watoto wao).
3. Kusoma vitabu, vijarida, kusikiliza vipindi vya kujenga akili siyo kubomoa. Usomaji ndo unaifanya kichwa kifanye kazi sana ile speed ya nerves inakuwa inaongezeka, kuna ile ukisoma na unastop mahali na kutafakari juu ya kile ulichokisoma, hapo ndo ndo unaongeza efficiency ya akili.
4. Usipende kukaa sehemu moja kwa muda mrefu, kwa mfano umekaa Dar kwa kipindi kirefu bila kutoka unaifanya ubongo usifikirie mapya, kuzunguka kwingi ndo akili inafanya kazi vizuri.

Yapo mengi lkn vikubwa ni hayo niliyoyaorodhesha hapo juu, yatakusaidia wewe kufikiri juu ya mazingira mbalimbali, kuyapitia mapitio mbalimbali kwa ufasaha kabisa na pia kuleta mchango mzuri kwa wengine katika majadiliano. Yote haya yatakufanya uongeze efficient ya akili vizuri, hayo yote yamewasaidia wenzetu wazungu kufikia pakle walipofikia. Yanayotubomoa sisi ni malezi mabomu.
 
Nafikiri inawezekana kutegemea na vitu gani tunaingiza kichwani kwa kusoma mfano vitabu, majarida nk na kusikiliza.

Tunaposoma mambo ya maana na kuishi katika mazingira ambayo tunakuwa tunasikia mambo ya msingi hata uwezo wetu wa kufikiri na kuhoji utaongezeka.

Tunayoyaongea mara nyingi yanareflect tunayoyafikiria hivyo unapoona mtu anaongea pumba tu muda wote ujue ata uwezo wake wa kufikiri ni mdogo.
 
du sijui mimi nafikiria nini hapa, vipi shehe yahya hajatoa utabiri mwingine
 
Tembelea hii website ya bbc BBC - Science & Nature - Human Body and Mind - Memory Tester

fanya hiyo survey na kujibu maswali na mwishoni wanakupa ushauri nini cha kufanya kuongeza au kuimarisha uwezo wako wa kufikiri, kumbukumbu na matukio.

Hapo ndo unaona tofauti ya wao na sie. Huo ni mfano mmoja lakini nadhani zipo njia na mbinu nyingi.

Nimewai kutaka kuiweka hii post hapa ikakataliwa na waendesha jamvi

Nice test. The question how often do you forget your partner’s birthday, men always forget.
 
Nice test. The question how often do you forget your partner's birthday, men always forget.

Hiyo test nilifanya nikagundgua mambo mengi sana na kuona wenzetu wanafonaya mambo kisomi . kwa hiyo ya birdhay inaonyesh wanaume we generaly dont care much . Mmbo mengi kuhusu wenzetu wa karibu awe gf, jirani ndugu au jamaa . Tofauti na wanawake.
 
The more you increase your knowledge, the more your thinking capacity will keep on increasing, the limit is you.
 
Yes! Read intellectual books everyday, eat healthy foods, exercise daily, listen to educative programs on the television, stop looking at programs that dont educate you and the first and foremost important thing is Fear God and feed yourself with His word daily.

He will give you the intelligence you need. Pia acha kusoma mageti ya udaku (Kama unasoma) soma informative newspapers.
kuna uwezekano wa binadamu kuongeza uwezo wake wa kufikiri,pls help
 
Uwezo wa akili kufikiri unachangiwa na mambo mengi na kuadhiriwa na baadhi ya mambo so far..

Mathalan uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo ni lazima uwe proportion na umri wa mhusika..Kutokana na upana wa hii maada ningefahamu umri wa mleta maada ingerahisisha sana wazo langu na kujua nilenge wapi shabaha isipotee..
 
Unaweza kuongeza uwezo wako wa kufikiri. But thoughts are things, then, at what measure do U want to develop/increase your things?
 
Uwezo wa akili kufikiri unachangiwa na mambo mengi na kuadhiriwa na baadhi ya mambo so far..
Mathalan uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo ni lazima uwe proportion na umri wa mhusika..Kutokana na upana wa hii maada ningefahamu umri wa mleta maada ingerahisisha sana wazo langu na kujua nilenge wapi shabaha isipotee..

Laiti kama ungelikuwa unasoma posts zilizotangulia ktk hii thread, usingelithubutu kutaka kupewa jibu la hapo penye nyekundu.
 
Back
Top Bottom