Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,933
- 988
Hapo ndy naanza kupata mashaka na uwezo wako wa kufikiri!
Nafikiri inawezekana kabisa wewe ndiyo ukawa na matatizo ktk uwezo wako wa kufikiri. Unataka kukimbia ukweli.
Rosemarie amejaribu kujitathmini akagundua mapungufu, anatafuta msaada ili awe bora. Kuonyesha uwezo wake kufikiri ulivyojuu ametambua kuwa kiini cha mapungufu ni namna anavyofikiri; hakusema ni kwasababu hana kitu fulani. Perfect evaluation. Huwezi kufanya kwa ubora hata kama tukikupa kila kitu lakini uwezo wako wa kufikiri ukiwa chini.
Amefanya kazi na wazungu akaiona tofauti aliyoandika. Ni mkweli. Hujamjibu umemshambulia kwa kushuku uwezo wake wa kufikiri. Si vema.
Kiukweli Rosemarie, unaweza ukafikiri sahihi kwa kiwango kikubwa kupita wanaume wa umri wako. Tena unawezakufikiri kupita wazungu. Ngoja tusubiri inputs za Invisible. Lakini nitachangia machache: ya kuwa vikwazo vingi vipo ktk namna tunavyolelewa na vingine vipo ndani yetu. Katika malezi tunayolelewa/tuliyolelewa
1. Hayatufundishi kuthubutu bali woga
2. Hayatufundishi kujiamini bali kuwa tegemezi
3. Hayatufundishi kuona kosa ni fursa ya kujifunza bali ndiyo mwisho (kushindwa)
4. Hayatufundishi kuitambua na kuithamini kazi ndogo/mafanikio madogo kuwa ni mtaji wa kutuchochea kufanya makubwa.
5. Hutufundisha kuona kufanya kazi kuwa ni utumwa wakati kazi ni utoshelevu wa maisha ya mwanadamu.
6. Hutufundisha kuona kuwa sisi hatuwezi ila wao/yeye anaweza, na wakati kuwa hata yeye hawezi kamwe.
Orodha ni ndefu.
Wengi wa wazungu tunaowaona kuwa ni bora ni kwasababu ya uzoefu, exposure, uthubutu na kujiamini. Ukifanyakazi hata na mtanzania aliyekuzidi katika eneo lolote ktk hayo mengine mko sawa mara zote utamwona bora .
Nitarudi.