Naweza kusoma Computer Science ikiwa Mathematics nina F?

Jaribu kuquote kwenye joining instruction yako uliyoweka hapo waliposema kujiunga na Computer Science lazima uwe na D ya hesabu. Nimetafuta sijaona.

Kumbuka mjadala wangu na mleta mada ulikua kwenye Computer Science na wewe umekuja kunipinga kuhusu kozi ya Computer Science.

Tubaki kwenye mada kuu wakati tunasubiri utuambie waliposema ni lazima uwe na D ya Maths.
 
Ndio unasoma vzuri kabisa. Unaanzia Certificate.

DMI wanakupokea vizuri tu.
Kwa nijuavyo mimi matokeo ya form 4 muhimu unapotaka kusoma degree.
Huwezi kuwa na F kwenye math ukakubaliwa kusoma Computer Science hata uanzie certificate , diploma kisha degree.

Akibahatika kupata nafasi hiyo atateseka sana na hesabu kwenye hiyo kozi huko University.
Akasomee vitu vingine au angalau IT anaweza akafanikiwa kufaulu.

Note: kuna tofauti kati ya IT Course na Computer Science Course kwa level ya degree.
 
Nimeshare experience yangu na DMI wanavyorecruit wanafunzi na wanavyofidia hilo gepu la Maths.

Can't prove no more.
 
Mimi nimesoma computer science.
Sikutishi nakupa ukweli usijepoteza muda.
Hiyo kozi kuna hesabu za maana.
Kama hesabu ulipata hivyo sababu zilikusumbua o-level hizo za chuo kikuu degree husika utakwama mapemaa kwenye Foundation of Mathematical Analysis na Descrete Mathematics.
Kuna Numerical Methods, Lenear Algebra, Logic and Semantics, Mathematical Modelling, na topic zingine nyingi tu.
 
Nimeshare experience yangu na DMI wanavyorecruit wanafunzi na wanavyofidia hilo gepu la Maths.

Can't prove no more.
Kozi ya bachelor degree ya IT, ICT, IS au Computer Science?
Hizo kozi tatu za mwanzo math siyo lazima uwe vizuri Sana.
Hiyo comp science ni lazima uwe na kuanzia D form 4. Ina hesabu ngumu ambazo mara kibao wanakamatwa sup freshman watu kadhaa waliofaulu Pure Math Advance Sec School.
 
Nadhani kuna shida mahali, na kama kweli una degree ya computer science basi itakuwa sawa na yule jamaa wa kitengo, Kitego gani? mambo ya system, system ipi? Mambo ya network. nimejaribu kukupa joining instructions ya hao hao ambao unajaribu kumdanganya mleta mada kuwa akienda DMI wao hawangalii hata kama un F. Bahati mbaya sana hata hiyo kozi ya computer engineering au computer science hawana. Pia hakuna chuo Tanzania hii ambacho wao wanautaratibu wao tofauti na ule wa NACTVET au TCU na joining instruction ndo hizo kama wewe ulifluke kipindi chako usimdanganye mleta mada. Au pia wewe lete ushahidi unaosema hata kama una F ya hesabu utasoma kozi husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…