kidonto
JF-Expert Member
- Jan 5, 2014
- 1,961
- 2,918
Huyo Jamaa ni Mjanja sana, Quebec ndo Jimbo pekee Canada ambapo Lugha rasmi ni Kifaransa! Ulivyosema alikutumia Documents zikiwa kwa Lugha ya Kifaransa, nikasema YES...!Ni kweli hao majamaa wa Lagos hawafai, japo nimeona nisikurupuke kwanza, niulizie uhalisia naona sasa nimpotezee tu kabla sijalizwa
Miaka 3 nyuma ilikua kidogo niende Quebec, nina rafiki pale, nilishaanza kujifunza mpaka Kifaransa, coz kwa aina ya Visa ambayo nilikua nataka, ningefanyiwa Interview na Ubalozi kama angalau namudu hata kujielezea kwa Kifaransa, sema safari yenyewe ikaingia Mdudu!
Naona Spirit yako, mimi nna uzoefu na mambo ya safari, ngoja nikupe idea....!
Zipo baadhi ya Nchi ambazo Zinaweza ku issue Visa yako huko huko kwenye hiyo nchi, Canada sio Moja wapo, kwa Canada kama una mwenyeji, yeye anachoweza kusaidia ni kukutumia barua ya Invitation, ambapo anakua amejifunga kukuhudumia wewe kipindi chote ukiwa huko, hasa kwa Visiting Visa, labda kukugharamia ticket ya go and return, na vitu vingine, hiyo barua ndo unaweza ku attach na Documents zako kwenda Ubalozini wewe mwenyewe kuomba Visa!
Ukiacha mipango yako ya kuomba ufadhiri wa masomo, tafuta Marafiki wa kizungu, tokea hapo hapo Quebec, tengeneza urafiki bila kuonyesha lengo lako, urafiki ukikolea, anza kuchomekea kuhusu Dhamira yako, mwambie rafiki yako, huitaji yeye akutumie pesa wala nini, unachoomba na akutumie tu mwaliko, na kwamba kuhusu ticket ya Ndege utagharamika mwenyewe, sidhani kama ticket ya ndege itakushinda, ukiweka nia, ndani ya miezi 3 ushapata rafiki tayari....!
Si lazima kuhangaikia Visa kubwa kubwa kama Resident Visa n.k....!Asante sana kaka [emoji120] ninalifanyia kazi hili
Hata ukipata Visiting Visa, kimbia haraka, uta renew mbele kwa mbele, na kutimiza ndoto zako.