Naweza nikamtibu mpenzi akaacha uongo?

Naweza nikamtibu mpenzi akaacha uongo?

Tiba nzuri ni KUMUACHA. Huyo mwanamke mwongo atakutesa maisha yako yote ukiendelea kuwa naye.
 
Huyu binti nampenda sana lakini anatabia ya kuongea uongo sanan kuna muda najipa imani kua ataacha lakini baada ya muda yanajirudia.

Shida nyingine hata ukimuuliza ni mgumu ku admit kwamba amekosean anahisi kama yuko katika nafasi ya haki kuongea alichoongea.

Nifanyeje? Moyoni nampenda ila akilini naona kabisa nitakua na mgogoro wa kimawazo sana kutokana na tabia yake.

1. Kuna aliwahi kua na mtu muongo na mwisho akaacha iyo tabia?
2. Kuna huduma ya counselling kuhusu hii tabia?
3. Kuna alieweza kudeal na hawa watu?
Tiba nzuri ni KUMUACHA. Huyo mwanamke mwongo atakutesa maisha yako yote ukiendelea kuwa naye.
huu ndio naweza kusema ndo ushauri sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama umeshamuambia na hapendi kubadilika yeye je unafikiri utaweza kumbadilisha wewe,?,

Hapo ndo unaposema ataacha ataacha mwsho wa siku ukishamuoa anazidisha mara kumi yake unakuja kuanza kulalamika Tena ,Kuna vitu ukishaviona wakati WA uchumber na vikawa havibadiliki unapaswa ukimbie .
hii ni kweli kabisa kwenye uchumba ukigundua mwenzako kuna vitu haviko sawa na wewe huwezi kuhimili ni bora mkaachana tu. maana akishaolewa ndo ana bweteka zaidi. it means mpaka umemua na udhaifu wake ameamini umeukubali udhaifu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachotakiwa ww nikuacha shobo ndio maana mtu anakuongopea usiwe mtu wakufunguka kila jambo kwake 😆
 
Hakuna dawa, Dawa ya kutibu tatizo hilo milele ni ww kuiweka nafsi yako katika hali ya utayari kua kila akisemacho uyo binti umpendae ni Ukweli mtupu,hta kama anasema uongo sbbu ww haugegedi uongo mkuu.
maisha ya uchumba + Mke ni tofauti na maisha ya mapisi kali wewe utapenda kudanganywa jambo mkuu? vipi unayajua madhara ya uongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu si umwambie kwamba mchumba wangu wewe ni MUONGO SANA, tatizo mnapenda mpaka mnashindwa kuwaambia hao mnaowapenda hata madhaifu yao mnakuja kulia lia humu

Simama naye mkiwa mnaangaliana mwambie wewe ni MUONGO pale utakapohisi kakudanganya asipobadilika timua mbio
 
Kama ulikaa chini kuongea nae kiutuuzima na akaendelea bas endelea kuvumilia hadi siku bomu likulipukie
 
Uongo wake ni upi mfano

Wakati mwingine nyie wanaume ni watu wa ajabu sana ukute mdada wa watu hataki uumie ana danganya

Mfano labda kila siku unauliza habari za umelala na wanaume wangapii?? Kwanini mliachana na ex wako

Aisee Hakuna mwanamke atajibu ukweli hayo maswali
 
Umegundua kwanini ni muongo? Kaa nae muulize na umwambie wazi pisi kali kama wewe hufanani kusema uongo.

Uongo na wizi ni watoto pacha wanaofanana kwa mbali.
 
Mtu akiwa anakudanganya ujue kuna namna anavyokuona kukuchukulia.

Sijui anakuonaje na anakuchukuliaje, ila anakudharau MNO.

Kimsingi umekumbatia bomu. Siwezi kukwambia ukimbie ili uliache lilipuke lenyewe, kwakuwa siwezijua unampango gani na maisha haya. Pengine unataka kufa na uwe shujaa! Tutajuaje?

Epuka dharau. Okoa maisha yako.
 
Inaonyesha hata mwanzo alikudanganya ana bikra,ila kufukua ukakuta bwawa.Tabia ni ngozi mkuu.
 
Back
Top Bottom