Naweza tumia Neutral kwenye mteremko?

Naweza tumia Neutral kwenye mteremko?

Habarini wandugu,
Je kuna madhari yoyote niki engage Neutral gear kwenye automatic transmission nikiwa nashuka mlima ili nisave wese?
Hautakiwi kabisa sababu gear shift ya auto hutegemea pressure ya oil hivo ukiweka free oil inakuwa haisukumwi, ukiweka D gafla gari italazimisha kusukuma oil nyingi sababu ya speed.
Auto sio kama manual unaeza kutoka 0 hadi gear no 5 bila kupita 1,2,3,4 auto huwa haivuki gear
 
kuna wengine mtu ana gari ndogo ya cc 1500 tu eti kwenye folen ya dakika 10 anazima gari OFF akiamin ana save wese.. jaman gari ya cc 1500 silencer wala hakuna wese kihiiivyo sawasawa una haribu stater tu na tena kuwasha upya unaanza shtua engine upya ndio unasababisha mafuta yaende mengi tu
 
kuna wengine mtu ana gari ndogo ya cc 1500 tu eti kwenye folen ya dakika 10 anazima gari OFF akiamin ana save wese.. jaman gari ya cc 1500 silencer wala hakuna wese kihiiivyo sawasawa una habiru stater tu na tena kuwasha unaanza shtua engine upya ndio unasababisha mafuta yaende mengi tu
Msiwapangie watu lita ya mafuta bei juu au nasema uongo Extrovert 😁😁😁
 
Habarini wandugu,
Je kuna madhari yoyote niki engage Neutral gear kwenye automatic transmission nikiwa nashuka mlima ili nisave wese?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] aliokuambia neutral inasave mafuta ni nani kaka? Pia hakuna dereva anaeshuka mlima gari ikiwa neutral maana gati inakuwa nyepesi sana na inazidi acceleration mara 2 ya ile iliokuwa nayo mwanzo kwa gari za automatic kuna muda mwingine brake zinajam na kuwa ngumu kukanyagika kwa manual transmission pia kuna muda zinakuwa ngumu ndio maana utakuta kwenye mlima lazima ushuke na gear tu brake za kunyunyiza
 
Madhara ya kushusha mteremko na neutral gear.

1. Unapoweka Neutral, unakuwa umeachanisha mfumo wa gear box na gari inakuwa free kumove bila gear inakwenda na msukumo wa uzito wake. Hii sio nzuri kwasababu gari itakuwa inakwenda kwa kasi bila kikomo na utakapotaka kuirudisha kwenye D utaipa stress ya kubalance gear na speed jambo ambalo utaipa shida gear box.

2. Gari inaposhuka kilima utataka kubalance speed kwa kukanyaga brakes. So utakuwa unaharibu brake pads zako bila sababu.

3. Mfumo wa gearbox ya gari automatic upo computerized kwa maana unacontrol speed, uzito, torque power, na clutch wenyewe. Kitendo cha kuweka neutral halafu gari ipo speed then ukaiweka D computer inakuwa disturbed na kuwa confused sababu ni kama umeiamsha katikati ya speed na itachanganyikiwa kupick gear na kumatch na speed.
 
Kwa gari ndogo tumia nyutro wakati unavutwa!!

Neutral ni burudani sana kwenye gari kubwa, kuna maeneo ukijiachia hahaha!
Yaani spidi unayoshuka nayo ndiyo hiyo hiyo unayopanda nayo..
 
Back
Top Bottom