Naweza vipi kuishi Pasina kuyatilia sana Maanani haya Maisha?

sawa, ila sasa hapo kwenye kusambaza furaha ndio changamoto. Furaha ni tunda la Roho Mtakatifu. huzaliwa kutoka ndani ya mtu. (moyoni).

kumpa mtu furaha, haiwezekani. ni ngumu sana kumridhisha mtu mwingine, haiwezekani.

YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI
 
Pole na Asante kwa mada fikirishi, binafsi baada ya kusoma nimejikuta nikiyatafakari maisha kwa angle nyingine. Kadri miaka inavyosonga ndivyo inavyokua ngumu kwetu kuyaishi maisha. Chuki, visasi, unafiki, tamaa, ubinafsi, majivuno vimekuwa vikiyatawala maisha ya kisasa.

Dhambi inatutafuna wanadamu bila ya sisi wenyewe kujua ni kiasi gani maisha yetu yanaathirika. Jiulize tuu nini kinaweza tokea kwa watu wa chini kiongozi anapokuwa mbinafsi, tujiulize ni athari ipi tunaipata kama jamii tunapokuwa na vijana wenye kuwaza anasa na zinaa siku nzima.

Zama hizi mtu akipata cheo ama pesa kidogo basi majivuno huibuka, wazee si wenye hekima tena. Kila mmoja anawaza namna kutimiza ndoto zake bila ya kujali kama njia inayoitumia inaweza leta athari kwa wengine. "What goes around comes back around" now days ni wangapi tunawaona machoni mwetu kuwa wamefanikiwa lakini hawana raha na maisha wanayoishi.

Mungu anatutaka kuishi kwa upendo, upendo na kumtegemea Mungu ndio njia pekee ya kuyapa thamani na maana maisha yetu apa duniani. Upendo unapotawala baina yetu majivuno, chuki, wivu, ubinafsi na tamaa hujitenga hivyo kuyapa udhati matendo yetu. Fikiria maisha yangekuwaje kama tungekuwa na jamii ambayo misingi yake imejengwa katika upendo na mshikamano.

Si jambo baya kujiwekea malengo, jambo la kuangalia ni malengo tunayojiwekea maana hayo yanaweza kuwa gereza katika maisha yetu hapa duani. Yana maana gani maisha yetu kama uwepo wetu apa duniani hautakuwa na baraka kwa wengine?
 
Ndugu katika yote uliyoandika ni mapito tu lakini maisha yako yapo katika kipande hicho kifupi hapo juu. Kamwe usitukuze huzuni kwani huzuni huuwa. Maandiko ya Biblia yanasema hivyo.

Mimi niliishi kwa mwaka mzima nikiwa na huzuni kubwa mno na kushindwa kulala zaidi ya masaa 3 na kweli nilijawa na hofu na kila kitu kiligeuka kuwa meaningless. Lakini nilipoweza kuacha kuweka mawazo yangu kwenye fears and failures, maisha yamekuwa na furaha hata kama bado sijapata nilichotaka matumaini ni mengi na naona kila dadili za kupata yote niliyoyapoteza.
 
Nashukuru kwa ku share mkuu, hakuna kukata tamaa na ushindi sio option ni lazima, tukaze.
 
upo uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana. Siku ukimpa Bwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…