Naweza vipi kurudi kwenye utumishi wa umma iwapo niliacha mwenyewe kazi?

Naweza vipi kurudi kwenye utumishi wa umma iwapo niliacha mwenyewe kazi?

Digital Ticha

Senior Member
Joined
Jun 16, 2023
Posts
183
Reaction score
266
Nikiacha kazi mwaka 2015 kutokana na sababu za kiafya na nikapokea mpaka mafao yangu ya PSPF.

Lakini sasa nimekuwa fit na naweza kufanya kazi kama kawaida.

Nilijaribu kuandika barua utumishi kuomba kurudi maana nilikuwa nikiomba kazi naambiwa nina check namba hivyo siwezi ajiriwa na mimi nataka nirudi kwenye utumishi.


Naomba ushauri kwa wanaofahamu utaratibu au waliowai kukutana na experience kama hii yangu.

Shukrani
 
Nimeelewa vyema ndugu mwalimu, unaweza kurudi japo process inaweza kuwa ngumu maana ulikuwa nje ya ajira karibu miaka 10+ na ndiyo maana nimekushauri jaribu upande wa pili

Au ulitakaje nieleweshe zaidi
😂😂😂😂
 
1. Nenda ofisi za tamisemi pale pmoja na utumishi onana na wakurugenzi wa wizara wa idara yako ya elimu wanaohusika..watakupa muongozo

2. Ukiona haviendi fanya mchakato wa kuonana na makatibu wakuu wa wizara hzo mbili (tamisemi na utumishi)

3. Hakikisha kuwa una vyambatanisho vyote vya matibabu yako

-Kama we ni mwalimu hususani masomo ya sayansi au biashara unaweza sikilizwa sana.

-epuka kuzua taharuki ya kuadai malipo mara hela ya kujikimu

NENDA UTUMISHI HOUSE PALE DODOMA AU TAMISEMI MJI WA SERIKALI MTUMBA.
 
Sio lazima urudi kazini
Tafuta namna nyingine ya kupata pesa
Nchi ina kila kitu vamia pori lolote utaona cha kufanya
Ukiahindwa sana tafuta mgodi ulio karibu yako nenda
Ukishindwa na hiyo nenda visiwani uingie kwenye uvuvi
Ukishindwa jiunge na kina heche muipiganie nchi.
 
Back
Top Bottom