Nawezaje ku recover email yangu?

Nawezaje ku recover email yangu?

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
4,072
Reaction score
12,119
Wadau mpo poa? Mwanenu hapa nahitaji msaada .
Niliibiwa simu yangu , baada ya muda nilipata nyingine . Changamoto ni pale ambapo katika ku log in kwenye simu mpya ikanihitaji nifanye 2 step verification. Kipengele kikawa kwamba namba niliyoisajilia hii email yangu kama verification ni ya vodacom . Namba hii kwa sasa sina , kuwapigia vodacom ili nifanye kui swap(renew) kupata hizo verification code, vodacom wakaniambia amepewa mtu mwingine yaani ishasajiliwa. 😬😬😬. Dah! Hapo nikachoka . Nikasema hebu nijaribu kufanya last option. Nikampigia huyo alepewa usajili kwa hii namba yangu ya zamani changamoto ni kwamba jamaa haelewi. Yaani nilimwomba anitumie hizo code za g_email(nikiwa online tayari nikiendelea na mchakato) ili mimi nifanye recovery huku kwenye simu niweze ku log in lakini amedinda , katakata na ni kama haelewi . Wadau nawezaje kuvuka hiki kiunzi..

NB: Email yangu na password naijua . Kipengele ni hapo tu kwenye two step verification.
 
Kwani si ufungue email nyingine tu
Bila shaka hiyo option anaijua ila email huwa zinabeba taarifa nyingi sana.

Hata mimi email yangu ina makitu yangu kibao, ikizingua huwa nafanya kila mbinu irudi.

Kwani mkuu mcTobby hukuweka recovery email?? Huwa kuna hiyo option ya kupata verification kupitia email yako nyingine.
 
Hapana niliweka tu namba
 
Of course nimefungua nyingine , ila ile ni ya muhimu sana kwangu mdau.
Usione wanakuambia hivyo wa tz wengi hawajajua umuhimu wa kutunza vitu kwenye email!, Mkuu lakini kuna option mbili zakupata msimbo sema ubovu huwenda hukufanya hiyo setting! unaweza kuziunga email mbili ama ktk namba yakupata msimbo ungeandika mbili!. hii husaidia sana.

Hapo kaa na huyo jamaa mlitatue na akikupa tu huo msimbo badili settings kwenye email yako chap.
 
Binafsi niki badili simu sina haja ya kuhamisha vitu maana niki jaza email tu vitu vyangu vinarudi vyote .ivyo email ni muhimu sana ,
 
Binafsi niki badili simu sina haja ya kuhamisha vitu maana niki jaza email tu vitu vyangu vinarudi vyote .ivyo email ni muhimu sana ,
Kabisa mkuu, miaka hii email ni ya kuilinda.
Na uzuri hizo settings huwa wanakusihi sana uzifanye ila kwakua wanakupa na option ya kuignore basi wengi wanachagua kuignore tu.
 
Hutaweza ku login kama hutapata hizo code , otherwise kama upate device ambayo ulishawahi kuingia kwa hiyo e-mail yako. Chakufanya fanya mchakato uonane na huyo mwenye hiyo lain japo atakuwa kijijinj sana
 
Usione wanakuambia hivyo wa tz wengi hawajajua umuhimu wa kutunza vitu kwenye email!, Mkuu lakini kuna option mbili zakupata msimbo sema ubovu huwenda hukufanya hiyo setting! unaweza kuziunga email mbili ama ktk namba yakupata msimbo ungeandika mbili!. hii husaidia sana.

Hapo kaa na huyo jamaa mlitatue na akikupa tu huo msimbo badili settings kwenye email yako chap.
Surely .. ndio najaribu kumpigia nione kama tutafanikisha lakini bado hapokei.
 
Hutaweza ku login kama hutapata hizo code , otherwise kama upate device ambayo ulishawahi kuingia kwa hiyo e-mail yako. Chakufanya fanya mchakato uonane na huyo mwenye hiyo lain japo atakuwa kijijinj sana
Unavyoniambia hapa upo sahihi asilimia 100. The only option ni hiyo ya ku settle hili swala na huyo mdau.
 
Oyaa sio powa man inabid tu nicheke kujifariji😂
Mimi ningekutoza hela tu ili nione upo serious kiasi gani hapo lazima ka ten kangekutoka ila kwa huyo jamaa hahahaha! hapo anaona sio tu unataka kumtapeli bali unaitaka na roho yake kabisa!, so vita inatoka kwenye msimbo mpk kufika hatua yakuanza kuvaa hirizi pumuzi...🤣
 
Back
Top Bottom