Hatumpi kisago wala nini...ila kiukweli ameacha au na kutengezza makovu ya kudumu katika mioyo yetu watoto wake kwa kitendo chake kile cha kutukimbia...
Ni yeye tu anakumbuka ule msemo wa mbegu ya haladari kwenye mafundisho ya biblia. Dingi alikuwa mseminari haswa ila kuna kisa kimoja kilimponza huko na akaachana kabisa na habari za kanisani. Hata Hata mimi niklikuwa mseminari sana, ila nikaambiwa utakuja kuwa kama baba yako, na nikapigwa chini kuendelea na habari za upadri. ni stori ndefu sana ndugu yangu, nimeadhibiwa sana kwa makosa ya mzee wangu na hili la kuadhibiwa haya yeye analijua. siwezi sema haya mambo humu maana yapo deep sana na ni ya familia.
Nili comment tu kumpa onyo mtoa mada kama yupo tayari watoto wake waadhibike au waadhibiwe kwa makosa ya wazazi wao... mimi ni living proof wa hili ambo.
Mama alikuwa hohehahe- primary school teach watoto 11 na akastaafu kwa lazima ya ugonjwa mwaka 1985 mimi nikiwa na miaka 9. Nikaanza la kwanza nikiwa 11 yrs kwa sababu mama hakumudu elfu 7 ya wakti huo, ingawaje wakati mwingine serikali muda huo ilikuwa inatupa madaftari bure huko primary school.
Baba akakimbia familia- -ugonjwa wa mama na hali ngumu ya Maisha- kufyatua wengi kunahusika.
watoto tukaishi kama kuku wa kienyeji- free range hadi tumetoboa sote na maisha ni safi.
baada ya kuona tumetoboa ndio sasa mzee anarudi kuomba msamaha- ni mtihani mkubwa sana.
Ilifika mahala sisi watoto tukawa tunajadiri namna ya kunywa sumu tuondokane na mateso ya dunia.
chakula kilikuwa taabu sana- chai ya rangi iliyotengezwa kwa mtama ilikuwa ya kugombania
wali ulikuwa unapikwa xmas pekee bila maharagwe au nyama na kwa jinsi tulivyo kuwa wengi ilikuwa ni sagura sagura ya uhakika, tonge moja tu na unaridhika.
haya mambo yasikie tu kwa wengine ndugu yangu. Niki- reflect nilipotokea, nilipo na ninapo jwenda , nazidi kumtukuza Mungu Muumba, maana alinipitisha katika yote na bila yeye, sijui kama ningekuwa hapa kuandika habari hizi. Nahisi hata unyonge kufikiria tu nilipo toka, ila kwa sasa, Namshukuru Mungu sana, na hawajahi kunitupa kwa kweli katika shida zangu zote - achana na habari hizi za dingi. Mungu yupo na ni wa kweli. Nimemuona katika maisha yangu ya utotoni, ujanani na sasa uzeeni nikikaribia kustaafu kazi.
Ni hayo. Pokea litakalo kufaa.